Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe Yusuph Mwenda akizungumza na wananchi wa kata ya Sinza leo hii wakati wa Uzinduzi wa ujenzi wa Kituo kipya Cha Polisi, katika Kata hiyo ambapo Mstahiki Meya huyo aliwataka wananchi wa Eneo hilo kutoa ushirikiano ili ujenzi wa jenngo hilo uweze kukamilika ambapo alisema kuwa zinahitajika zaidi ya milioni hamsini ili jengo hilo liweze kukamilika. Aidha Meya huyo alisema kuwa kwakuhakikisha kuwa ulinzi wa unaimarika maeneo ya Sinza, atahakikisha kuwa Mitaa yote 53 iliyopo Sinza iajengwa vituo vya Polisi. Katika milioni 53 zinazo hitajika kujenga kituo hicho cha polisi tayari Mbunge wa jimbo la Ubungo amechangia Milionio Kumi kutoka kwenye mfuko wa Jimbo. |