Mgombea
wa Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya yanga Bw, Ayubu Nyenzi akizungumza na
waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam alipokutana na waandishi wa habari
akaamua kuelezea nia yake ya kugombea kiti hicho ambapo alisema kuawa anataka
agombee ili awahase wanachama wa yanga kuchanga 5000 kila siku kwa ajili ya
kumaliza matatizo yaliyopo klabuni hapo na sio kutegemea misaada kutoka kwa
wafadhili. Alisema kuwa endapo wanachama watatoa Sh, 5000 kila mmoja
zitapatikana kiasi cha sh, milioni 70 kwamwezi. |