Tuesday, June 26, 2012

SIKU YA KUPINGA MADAWA YA KULEVYA KITAIFA YAFANYIKA LEO JIJINI DAR

WAZIRI wa Mambo ya ndani Dk Emanuel Nchimbi akisoma hotuba badala ya Waziri mkuu Mhe, Mizengo Kayanza Peter Pinda Kwenye Maadhimisho ya siku ya kupinga Matumizi ya madawa ya Kulevya Duniani ambapo kitaifa nchini Tanzania yalifanyika leo Kwenye viwanja vya shule ya msingi Tandale jijini Dar es Salaam ambapo hotuba hiyo ilielezea namna itakavyo pambana na kudhibiti madawa ya kulevya ikiwa ni pamoja na kudhibiti kusafirishwa ambapo waziri alisema kuwa wameweka askari kwenye njia zote ambazo wanaweza kupitisha madawa ya kulevya. Aidha hotuba hiyo ya waziri mkuu iliwataka pia wakulima wanao husika na kulima Bangi, Mirungi na madawa mengine kuacha mara moja kabla hawajakutwa na vyombo vya dola.
Baadhi ya waathirika wa madawa ya kulevya ambao tayari wameacha kutokana na msaada wa dawa ya Methadone anayopewa mtumia madawa aya kulevya, ili aweze kuacha madawa ya kulevya wakiwa wameshika bango la Kutaka serikali iwasaidie kupata dawa hiyo ya Methadone kwa urahisi.
Baadhi ya washiriki mbalimbali wanaopinga matumizi ya madawa ya kulevya  wakishangilia uwepo wa waziri kwenye maadhimisho hayo.
Muhogo mchungu naye alikuwepo kwenye maadhimisho hayo akiwa kwenye picha na baadhi ya waathirika wa madawa ya kulevya.
Baadhi ya madawa ya kulevya yanayowaharibu vijana na kusababisha kupoteza nguvu ya Taifa.
Msanii Wilbert Mpanda maarufu kama Wille B ambaye naye alikuwa mtumiaji wa Madawa ya kulevya akiimba wimbo wa kuelimisha wenzake ili waache madawa hayo.