Tuesday, June 12, 2012

SERIKALI YAPEWA ONYO NA VIONGOZI WA DINI; WASEMA WANAPOTEZA TRILIONI 3 KILA MWAKA

Mwenyekiti wa kamati ya Viongozi wa Dini  iliyokuwa inafanya uchunguzi juu ya upotevu  wa mapato ya Serikali Askofu mkuu wa jimbo la kuu la Tabora   Paul Ruzo akizindua Uchunguzi huo bada ya kukamilika ambapo alisema kuwa Serikali ya Tanzania inapoteza kiasi cha shilingi Trilioni Tatu kila mwaka katika sekta mbalimbali ikiwemo Misamaha ya kodi kwa wawekezaji pamoja na utoroshwaji wa mali kwenda nje ya nchi bila kulipia.Askofu Ruzo alisema kuwa Watanzania wengi wanaishi katika hali ya umasikini kutokana na serikali kupoteza kiasi hicho cha pesa kila mwaka hivyo ameitaka serikali kuwa makini sana katika sekta hizo hasa za kodi.

 Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa kamati ya Viongozi wa Dini  iliyokuwa inafanya uchunguzi juu ya upotevu  wa mapato ya Serikali Askofu mkuu wa jimbo la kuu la Tabora   Paul Ruzo katikati ni Hassan Fariji Sheik Mkuu  mkoa wa Mwanza ambaye ni Makamu mwenyekiti wa kikao na wamwisho kushoto ni Askofu Stephen Munga ambaye ni mjumbe wa Kamati kwa pamoja wakiwa katika uzinduzi huo.
Baadhi ya wajumbe kutoka sehemu mbalimbali katika uzinduzi wa uchunguzi huo.

Askofu Paul Rizo (katikati) pamoja na Sheik Hussen Fariji wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa uchunguzi huo.

Askofu Paul Rizo (katikati) Sheik Hussein Fariji (kushoto) wakionyesha ripoti hiyo ya uchunguzi baada ya kuzinduliwa kulia ni Dkt, Prosper Ngowi Mkufunzi Chuo kikuu cha Mzumbe ambaye ni mmoja kati ya waliofanya uchunguzi huo.