Friday, June 22, 2012

RIGHT TO PLAY YAMALIZIA MAFUNZO YAKE LEO

Mfunzo ya michezo yaliyoandaliwa na Right to Play yanafikia ukingoni leo baada ya kuanza jana katika Ukumbi wa Ubungo plaza jijini dar es Salaam.

Director wa British council akizungumza katika semina ya Right to play ambapo alielezea jinsi michezo inavyo weza kuwaleta watu pamoja na namna michezo inavyoweza kuendelea kulinda amani kama ikipewa nafasi katika maisha ya Binadamu.
Raisi wa Olympic Tanzania Mhe, Gulam Rashid akichangia mada katika semina hiyo inayoendelea leo katika ukumbi wa Ubungo plaza jijini Dar es Salaam.

Naye Katibu wa Ngumi Tanzania Bw, Makore Mashaga , alikuwepo ambapo aliuliza ni kwanamna gani mchezo wa Ngumi unashirikishwa na kutangazwa na Asasi hiyo ili kukuza mchezo huo.

Meneja Uwezeshaji wa Right To play Bw,Francis Rwiza akijibu maswali kutoka kwa waandishi wa Habari kuhusiana na semina hiyo ambayo inaisha leo.