Bonanza
kubwa la mchezo wa mpira wa miguu linaloitwa 'Nane nane soccer bonanza'
linatarajiwa kufanyika kwenye viwanja vya Tanganyika Parkers Kawe jijini
Dar es Salaam siku ya kilele cha sherehe za nane nane.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa kampuni ya SULE'S INC. &
ENTERTAINMENT, Salum Suleiman ambao ndiyo waandaaji wa Bonanza hilo timu
mbalimbali kutoka katika maeneo ya wilaya ya Kinondoni jijini Dar es
Salaam zitashiriki.
"Maandalizi ya bonanza
hili yameshafikia katika
hatua nzuri kabisa, Kamati imefanya kazi nzuri mpaka kufikia hapa na
tunategemea bonanza hili litafanyika kwa mafanikio makubwa,"alisema
Suleiman.
Akizungumzia timu zitakazoshiriki
katika bonanza hilo, Suleiman alisema,"tunatarajia kuwa na timu nane
ambazo zitachuana katika kuwania kombe siku hiyo na mashindano
yataendeshwa kwa mtindo wa mtoano."
Alisema
wameamua kuliendesha bonanza hilo kwa mtindo wa mtoano ili timu ziweze
kutoa ushindani wa kutosha na kuburudisha watu watakaojitokeza katika
bonanza hilo.
"Washindi watapata zawadi, kwa
sababu mshindi wa kwanza atatwaa kombe, mshindi wa pili pia atapata
zawadi, mchezaji bora, mfungaji bora, kipa bora na mchezaji mwenye
nidhamu wote hao watapata zawadi."
Sherehe za nane hufanyika kila mwaka sehemu mbalimbali nchini ikiwa ni siku ya kuadhimisha siku ya wakulima.