Mbunge wa Jimbo la Segerea, Dk. Makongoro Mahanga (kulia), Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa (kushoto) na Mwenyeji wa harambee ya kuchangia mpango wa elimu wa Kata ya Kipawa, Diwani wa Kata hiyo Bonah Kaluwa, wakimuongoza Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa ambaye alikuwa mgeni rasmi kuingia ukumbini.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Shinyanga, Hamisi Mgeja (katikati) akipongezwa na Mgeni rasmi wa harambe hiyo baada ya kuchangia sh. 500,000.
Diwani wa Kata ya Kipawa Bonah Kaluwa (katikati) wakibadilishana mawazo na mgeni rasmi kulia na kushoto ni meya wa manispaa ya ilala Jerry Silaa.
Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa (kushoto), akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh.milioni 10, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, aliyekuwa mgeni rasmi katika harambee ya kuchangia mpango wa elimu Kata ya Kipawa, iliyofanyika Dar es Salaam jana usiku katika hoteli ya Kempiski jijini Dar. Fedha hizo zilitolewa na Manispaa hiyo ambapo zaidi ya sh. milioni 400 zilipatikana.
Mgeni rasmi wa harambee hiyo Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa (wa
pili kulia), akiwa amesimama na viongozi wa Chama cha Mapinduzi na
Manispaa ya Ilala wakati wimbo wa taifa ukipigwa kabla ya kuanza kwa
harambee hiyo.
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye harambee hiyo
Diwani wa Kata ya Kipawa Bonah Kaluwa, akitoa neno la shukurani kabla ya kuanza kwa harambee hiyo.
Mgeni rasmi wa Hharambee hiyo akimpa mkono wa asante mwakilishi wa kampuni ya Home Shopping Centre Bi Madiha Al Harthy (kushoto),Salma baada ya kuchangia sh. milioni 22.
Mkurugenzi wa SONGAS Limited Bw;Christopher Ford(katikati),akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya dolla za kimarekani 10,000, mgeni rasmi wa harambee hiyo.kushoto meneja rasilimali Songas Bi Agatha Keenja.