Saturday, June 9, 2012

MEYA WA KINONDONI AFUNGUA MAONYESHO YA TANZANIA HOMES EXPO JIJI9NI DAR


Picha na Evalyn Shayo
Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe, Yusuph Mwenda (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa maonyesho ya wadau wa kukopesha nyumba (Tanzania Homes Expo) kupitia benki mbalimbali nchini, ambapo wananchi wanaonyeshwa urahisi wa kuweza kukopa nyumba. Maonyesho hayo yamefanyika leo katika viwanja vya Mlimani City jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Uandaaji wa maonyesho hayo Tanzania Homes Expo Bw, Zenno Ngowi.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe, Yusuph Mwenda, akipewa maelezo katika banda la Benki ya Akiba Commercial wakati akitembelea Kampuni zilizoshiriki katika maonyesho hayo.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe, Yusuph Mwenda, akikagua baadhi ya makabrasha katika banda la Shirika la nyumba Tanzania Nhc kushoto ni Afisa masoko wa Shirika hilo Mariam Iddi na kulia ni Afisa mauzo mwandamizi wa shirika la nyumba Tanzania (NHC) Bw, Emanuel Lymo.
Meya wa manispaa ya Kinondoni Mhe, Yusuph Mwenda (kulia) akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na maonyesho hayo na kushoto ni  Mkurugenzi wa Uandaaji wa maonyesho hayo Tanzania Homes Expo Bw, Zenno Ngowi.
Mkurugenzi wa Uandaaji wa maonyesho hayo Tanzania Homes Expo Bw, Zenno Ngowi akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari juu ya maonyesho hayo ambapo alisema huo ni mwanzo tu na wanatarajia kuendelea kuonyesha kwa miaka mingine ijayo.