Wednesday, June 27, 2012

KAMANDA KOVA AZUNGUMZIA UTEKAJI WA DK OLIMBOKA

 Kamanda wa polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam  Suleiman Kova akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio la utekaji nyara na kujeruhi lililompata kiongozi wa jumuiya ya Madaktari Dk Steven Ulimboka anayedaiwa kutekwa na kujeruhiwa vibaya na  watu watano wakati akipata kinywaji katika klabu ya Leaders Kiondoni jijini Dar es salaam. Kamanda Kova amesema Ulimboka aliokotwa na msamaria mwema ambaye hakutaka kumtaja jina lake kiusalama na kutoharibu upelelezi.