Thursday, June 28, 2012

COCACOLA NA TASWA KUTOA TUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO

Mkurugenzi wa Maasiliano ya Umma  Kampuni ya Cocacola Bw,  Evans Mlewa akizungumza na waandishi wa habari leo hii jijini dar es Salaam kuhusiana na Tunzo watakazokuwa wanazitoa kwa waandishi wa habari ambapo kwa kushirikiana na Chama cha waandishi wa habari za michezo TASWA  watatoa zawadi kwa  waandishi wa habari za michezo walioandika vizuri kuhusiana na Michuano ya Copa Cocacola. Alisema kuwa Zawadi hizo zitatolewa kwa waandishi kutoka kwenye vyombo mbalimbali ambvyo alivitaja kuwa ni TV,Radio, Magazeti  pamoja na Mitandao ya Kijamii kama Blogu.Aliongeza kuwa kila mwandishi atapeleka vipindi vyake au stori alizoziandika katika ofisi za Cocacola na Mshindi katika kila chombo atapatiwa kiasi cha shilingi Milioni Mbili za Kitanzania.

Katibu Msaidizi wa TASWA Bw, George John (kulia) akielezea sifa za stori pamoja na picha zitakazokuwa zinahitajika katika mashindano hayo ambapo alisema kuwa lazima stori na picha zote zifwate maadili ya kiuandishi.

Mkurugenzi wa Maasiliano ya Umma  Kampuni ya Cocacola Bw,  Evans Mlewa (katikati) na kulia ni Katibu Msaidizi wa TASWA Bw, George John wakisikiliza kwa makini maswali ya waandishi wa habari kuhusiana na Tunzo hizo kushoto  ni Meneja mauzo wa Cocacola Tanzania Bi, Salome Babirizi.