Wednesday, June 27, 2012

MWENYEKITI WA JUMUIYA YA MADAKTARI AVAMIWA NA KUUMIZWA VIBAYA NA WATU WASIOJULIKANA.

 Daktari kiongozi wa jumuiya ya Madakta Tanzania  Dk. Steven  Ulimboka alivyokutwa na kituo cha sheria na haki za binadamu baada ya kutolewa kituo cha polisi BUNJU. Dk Ulimboka alikutwa katika mji mpya wa Mabwepande akiwa amefungwa kamba na watu wasiojulikana  mikononi leo katika majira ya hasubui akiwa hoi. Jmbo hilo limetokea wakati Madaktari nchini hasa wa hosipitali ya Muimbili wakiwa katika mgomo kuishinikiza Serikali kuwapa haki zao na Dk Olimboka ndiye Kiongozi wa Mgomo huo.

Dk Akinywa maji kama  huduma ya Kwanza baada ya kutolewa polisi Bunju..

Baada ya kufikishwa Hosipitali Waandishi wa habari hawakupewa nafasi ya kumpiga picha kutokana na kuzuiwa na baadhi ya Askari  wanaoonekana ni baadhi ya waandishi wa habari wakifanya jitihada zote kuweza kupata picha.

Kwa mbali mpiga picha wa MAASINDA aliweza kupata namna alivyofunikwa wakati akipelekwa  Kwenye kitengo cha Mifupa MOI baada ya mwili wake kufanyiwa uchunguzi. pichani ni baadhi ya watu wasiojulikana kuwa ni wahudumu wa hosipitali au ni askari wakimfunika Dk Olimboka.