Msanii wa Uganda, Jose Chameleone (kulia) leo
amekamilisha taratibu zote za kusaini mkataba wa kufanya shoo kali Uwanja wa
Taifa mpya, jijini Dar es salaam, siku ya sabasaba baada ya Meneja Mkuu wa
Global Publishers, Abdallah Mrisho, kutia timu Entebe mapema leo. Pichani chini
ni Chameleone akijigamba kufanya shoo na akisaini mkataba wa mwisho huku
akishuhudiwa na meneja wake. Chameleone ametoa onyo kwa Diamond kuwa
atamchakaza na Valuvalu!
|