Hali ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk.
Stephen Ulimboka, inaendelea vizuri katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es
Salaam alikolazwa jana baada ya kutekwa, kupigwa na watu wanaodhaniwa
kuwa majambazi.
Tetesi tulizozipata kutoka kwa wadau wetu, kutoka Muhimbili usiku wa
kuamkia leo, zimedai kwamba Dk. Ulimboka aliweza kunywa mtori aliopelekewa na
madaktari wenzie.
Pia, ilielezwa kuwa waodi aliyolazwa ilikuwa na ulinzi mkali wa madaktari
wenzie, ambapo hakuna mtu yeyote asiyefahamika kusogea ama kuingia
kumuona.
|