WAZIRI
wa Viwanda na Biashara Mh, Abdala kigoda akiongea na wajumbe pamoja na Viongozi
wa kiwanda cha Urafiki alipotembelea kiwanda hicho leo
jijini Dar es Salaam ambapo aliziona changamoto nyingi pamoja na ufisadi unaofanyika kiwandani hapo baada ya wafanyakazi kumueleza namna wanavyo kandamizwa na wachina ambao ndio viongozi wa kiwanda hicho ikiwemo mishahara midogo ya wafanyakazi na akaahidi kuzifanyia kazi.
Diwani
wa kata ya Ubungo jijini Dr es Salaam Mh, Bonifas Jacob
akieleza changamoto zinazo wakabili wafanyakazi wa kiwanda hicho pamoja na
usimamiaji mbovu wa Kiwanda hicho mbele ya Waziri.
Baadhi
ya wafanyakazi, Viongozi pamoja na wajumbe mbalimbali waliohudhuria kwenye
ziara hiyo wakimsikiliza Mh, Waziri kwa umakini.
Naibu
Meneja uchapishaji na utiaji rangi kwenye kanga Bw, Solomon Laban(kulia)
akimuelekeza waziri namana mtambo huo wa utiaji Rangi unavyofanya kazi
akikagua baadhi ya Mitambo ndani ya kiwanda hicho.
Waziri
akikagua uzalishaji wa kanga kiwandani hapo.
Mh,
Waziri wa viwanda na Biashara akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa
kiwanda hicho baada ya kumaliza matembezi.