Friday, May 18, 2012

MBUNGE VITI MAALUM AAHIDI KULIVALIA NJUGA UZEMBE WA HOSIPITALI YA AMANA

 MBUNGE viti maalumu kwa tiketi ya chama cha Demcrasia na Maendeleo chadema Mh, Philipa Mturano akizungumza na wazazi wa mtoto aliyezaliwa akiwa (hawapo pichani) amesimama katika Hosipitali ya Amana iliyopo jijini Dar es Salaam kutokana na Uzembe na kutokuwa na umakini kwa wakunga wa Hosipitali hiyo ambapo Mturano alilaani vikali kitendo cha muuguzi aliyekuwa zamu siku hiyo kutomsaidia mama huyo aliyefahamika kwa jina la Kuruthum Abdallah kwa kutaka kumchelewesha na kusababisha mama huyo kujifungua akiwa amesimama na kichanga kudondoka Sakafuni. Mwanamke huyo aliyejifungua akiwa amesimama anatoka katika manispaa ya Ilala kitongoji cha Majohe jijini Dar es Salaam
Mbunnge Philipa akiwa amekishika kichanga hicho kilichonusurika kufa, Philipa aliitaka Serikali kumchukulia hatua za kisheria muuguzi huyo ikiwa ni pamoja na kuchunguzwa kama vyeti vyake ni vya halali pamoja na kumfukuza kazi.
Philipa akiwa na Mtpto Arafa aliyenusurika kufa baada ya kuangukia sakafuni wakati anazaliwa.