Wednesday, May 16, 2012

TCRA YASHEREHEKEA SIKU YA MAWASILIANO DUNIANI

 Katibu mkuu wa wizara ya Mawasiliano  Sayansi na Teknolojia Dr Florens Turuka akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku mbili kuelekea kilele cha siku ya sherehe ya mawasiliano duniani ambapo maadhimisho hayo yanatarajiawa kufanyika kesho Duniani kote, Dk Turuki amewaomba wafanya biashara wauze televisheni ambazo zipo katika mfumo wa Digital. Warsha hiyo imefanyika leo hii katika Ukumbi wa Mamalaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA Jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya mawasiliano Tanzania Prf, John Nkoma akizungumza na waandishi wa habari  leo hii jijini Dar es Salaam kwenye Semina inayoambatana na Sherehe ya  siku ya mawasiliano Duniani. ambapo amewataka watanzania kuelewa umuhimu wa mawasiliano ya mtandao.
 Baadhi ya wadau mablimbali wa mawasiliano nchini waliohudhuria kwenye warsha hiyo.
 Mwanafunzi wa shule ya Msingi  Mapinduzi Zuwena Muddy, akitoa mafunzo ya namana ya kutumia Computer  kwa wadau waliohudhuria kwenye semina hiyo.
Mwanafunzi Jackson Joseph kutoka shule ya Msingi  Mapinduzi jijini Dar es Salaam manispaa ya Ilala, akihojiwa na waandishi wa habari juu ya faida ya matumizi  ya Computer.


Mwanafunzi Zuwena Muddy akisisitiza mafunzo hayo kwenye warsha hiyo.