Mpaka hivi sasa watu wamezidi na wanaendelea kuzidi kuongezeka kwenye mazishi ya msiba wa aliyekuwa nguli wa fiolamu nchini Steven Kanumba.
Kwa namna MAASINDA ilivyopita imeshuhudia watu wakiwa wengi na wengine wanakosa hata mahali pa kukaa.
Wengi waliomo na walio weahi kufika katika msiba huu ni wapenzi wa filamu na wale wasanii wanaochipukia.
Kwa taarifa ambazo MAASINDA imepata ni kwamba mke wa raisi Mama salma kikwete atahudhuria mazishi hayo ambayo yatafanyika kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Mazishi ya Kanumba yanafanyika kabla polisi haijatoa tamko rasmi kuhusu hasa ninini kilicho muua msanii huyo.
Hivi karibuni Kamanda wa polisi mkoa wa kinondoni Charles Kenyela alikaririwa akisema kuwa, wanasubiri ripoti ya Madaktari kuhusiana na kifo cha kanumba.
Swali ni kwamba, Mazishi yanafanyika leo je, madaktari wataendelea kuchunguza nini? kama wamemaliza mbona hawajatupa ripoti kamili?