Saturday, April 21, 2012

UVUMI WA MITANDAO YA KIJAMII KUHUSU KUJIUZULU KWA MAWAZIRI WALIOTAJWA KUWA NI WEZI



 KUTOKANA na uvumi ulioenea usiku wa kuamkia leo huko Dodoma kufuatia shutuma za wabunge dhidi ya mawaziri kadhaa wa Wizara wanaotuhumiwa kutowajibika vya kutosha na kutuhumiwa kwa wizi katika wizara wanazoziongoza, usiku wa mkuamkila leo Katibu wa wabunge wa CCM bungeni mama Jenista Muhagama amewaambia waandishi wa habari kwamba ni kweli walikuwa na kikao na wamechukua maamuzi magumu, lakini yeye siyo msemaji wa suala hilo hivyo huenda taarifa zaidi zitatolewa ufafanuzi wakati wowote kuhusu suala hilo,  msemaji  wa wabunge wa CCM Bungeni ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

Wabunge wa CCM walichachamaa sana katika suala hili na wamelivalia njuga  vyakutosha wakipaza sauti kwamba lazima mawaziri hao wawajibike, tutawaletea taarifa zaidi kadiri tutakavyozipata. 




 UVUMI WENYEWE ULIOKUWA UMEENEA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII NI HUU
20/04/2012
2 Comments

Ni taarifa zinazosambaa katika mitandao jamii ya Facebook, Twitter kwenye eGroups na eForums. Taarifa hizi zinatofautiana na kwa kuwa hazijathibitishwa kwa namna yoyote ile, zitabaki kuwa TETESI tu. Ikiwa ni kweli itafahamishwa hivyo, ikiwa ni uongo, basi na tetesi hii ipuuzwe!

    Zitto Zuberi Kabwe @zittokabwe

    Press conference ya ministers kujiuzulu inaendelea
    20 Apr 12

        * Reply
        * Retweet
        * Favorite

Unaweza kufuatilia mwenyewe kwenye ukurasa wa "Habari" kwenye menu juu utaona vijisanduku vya Twitter yenye tweets za Watanzania, JamiiForums, MabadilikoTanzania na Wanabidii.

Mojawapo inasema: "Wanaotajwa kujiuzulu ni Mkulo-Fedha, Dkt. Chami - Viwanda na Biashara, Dkt. Mponda - Afya na Nundu - Uchukuzi. Inasemekana watatoa tamko usiku wa leo."

    Joseph Msendo @msendo4life

    Breaking News ya Radio One, inasemekana mawaziri 8 wamejiuzulu..
    20 Apr 12

        * Reply
        * Retweet
        * Favorite

    Nathan Chiume @chiume

    Unconfirmed reports of forced resignations of 8 ministers in #Tanzania by MPs from ruling caucus after opposition no confidence vote threat
    20 Apr 12

        * Reply
        * Retweet
        * Favorite

    Edward Mhina @Mgossi

    RADIO ONE Breaking News: Inasema kwamba... Mhe.Jenista Mhagama ansema Wabunge wa CCM Wamefanya MAAMUZI MAGUMU usiku huu. Lakini HAJAFAFANUA!
    20 Apr 12

        * Reply
        * Retweet
        * Favorite

    Zitto Zuberi Kabwe @zittokabwe 20 Apr 12

    @Thuwein I claim no credit at all. Tunatimiza wajibu wetu. Players wengi, it was a teamwork @Semkae @Irenei2011 @iMashibe @AnnieTANZANIA

    Mbaraka Islam @Islam_Dar

    @zittokabwe @Semkae @MariaSTsehai @iMashibe Mkulo,Chami,Ngeleja, Nundu, Maige, Mkuchika, Maghembe Mponda barua usiku huu @ChangeTanzania
    20 Apr 12

        * Reply
        * Retweet
        * Favorite

Nyingine inasema: " Mawaziri hao ni; Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, Waziri wa Viwanda na Biashara, Cyril Chami, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, Waziri wa Uchukuzi, Omar Nundu, Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Mkuchika, Waziri wa Kilimo Chakula na Ushurika Jumanne Maghembe na Waziri wa Afya, Dk. Haji Mponda."

Sababu ya kujiuzulu inatajwa kuwa ni ili kumnusuru Waziri Mkuu na taratibu nyingine zinazochukuliwa pale Waziri Mkuu anapojiuzulu.A