Monday, April 23, 2012

BALOZI SEIF ALI IDDI ASEMA NCHI ZA AFRIKA ZISHIRIKIANE KUTATUA TATIZO LA MAJI

MAKAMU wa pili wa rais wa Zanzibar Balozi Seif Alli Iddi amezitaka nchi za Africa  kuwa na ushirikiano katika kutatua tatizo la maji katika nchi za Afrika.


Aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam katika hotuba yake wakati akifungua  mkutano ulioandaliwana  shirika la maji la UNESCO wa kujadili namna ya kutatua changamoto katika sekta ya maji nchini na Barani Afrika.


Balozi Seif alisema kuwa ili kutatua changamoto zinazoikumba sekta ya maji ni lazima kuwepo na ushirikiano katika nchi zote za afrika kwani karibu nchi zote za afrika zinakumnbwa na tatizo la maji.


"Ni karibu nchi zote za afrika zinakumbana na Tatizo la maji na ili tuweze kulitatua tatizo hili, ni lazima nchi zote zikaamua kufanya kazi kwa pamoja ili kutatua tatizo hili",alisema Seif.


Aliendelea kusema kuwa, anategemea ifikapo mwka 2025 iwe tatizo la maji limekwisha katika nchi za Afrika na hii itawezekana kama kukiwepo na ushirikiano kwa nchi zote zenye tatizo la maji.


"Tunategemea ifikapo mwaka 2025 kuwe hakuna tena matatizo katika sekta ya maji nchini na barani afrika kwa ujumla", aliongeza.


Mkutano huo ulihudhuriwa na wajumbe 60 kutoka nchi 22 za barani Afrika waliojitokeza kujadili changamoto hizo katika sekta ya maji.


Baadhi ya nchi hizo ni pamoja na Zambia,Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo,Nigeria, Mali, Niger, Benin, Botswana, Cote Divore, pamoja an Senegal.


Nchi nyingine ni pamoja na Ghana,Kenya, Uganda, Swaziland,Burundi Malawi na Tanzania.