Jeshi
la Polisi Zanzibar linamshikilia mwanamke mmoja mkazi wa Tomondo mjini
Zanzibar kwa tuhuma za kuiba mtoto mchanga mwenye umri wa miezi mitano
kutoka katika Hospitali Kuu ya Mnazimmoja mjini Zanzibar.
,Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi Zanzibar, amemtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Fatma Abdallah Mohammed(26)
ambaye alikamatiwa Bandarini akisafiri na mtoto huyo kwenda Pemba.
Kamanda
Aziz amesema kuwa mtoto huyo aitwaye Aisha Nassor Ali, aliibwa Aprili
10, mwaka huu majira ya saa tano asubuhi wakati mama wa mtoto huyo Bi.
Rahma Hassan Ali, alipompeleka mtoto wake kupata matibabu katika
Hospitali ya Kuu ya Mnazimmoja mjini Zanzibar.
Amesema
wakati mama wa mtoto huyo akiwa katika foleni ndefu ya kutaka kupata
kadi ya kumuona daktari, alitokea mwanamke mwingine ambaye sasa ni
mtuhumiwa, akijifanya kuwa ni mwandishi wa Habari na alikuwa akifuatilia
kezo za tiba katika Hospitali hiyo, lakini pia alikuwa akifahamiana na
mmoja wa madaktari na hivyo kumtaka ampe msaada ili mtoto huyo aweze
kupatiwa tiba kwa haraka.
Amesema
mtuhumiwa huyo aliongea na simu na kujifanya kuwa alikuwa akionge na
daktari na bwamba amemtaka apelekwe mtoto huyo kwake kwa matibabu na
ndipo mtuhumiwa huyo alipomwambia mama wa mtoto kuwa ampatie mtoto ili
atangulie naye kwa daktari na kumtaka mama wa mtoto akatafute daftari la
kuandikia matibabu ya mtoto wake.