SHIRIKISHO la Filamu Nchini (TAFF),
limesema litamchukulia mtu yeyote hatua za kisheria atakayebainika kuuza
CD za shughuli za mazishi ya marehemu Steven Kanumba bila ridhaa ya
familia.
Tamko hilo lilitolewa jana na Rais wa
TAFF, Simon Mwakifamba katika mkutano wake na waandishi wa habari,
nyumbani kwa marehemu Sinza Vatican jijini Dar es Salaam ambapo lengo
lao ilikuwa ni kutoa salamu za shukrani kwa wote waliohudhuria msiba
huo.
Mwakifamba alisema tayari wameshapata
taarifa za watu kuanza kuuza cd hizo kwa lengo la kujipatia fedha jambo
ambalo sheria ya filamu hairuhusu.
Kwa mujibu wa Rais huyo, Kanumba alikuwa
akitegemewa na familia yake kupitia kazi za filamu ambapo sasa hivi
kutokana na kutokuwepo kwake familia itayumba.
Hivyo alisema endapo CD hizo zitaweza
kusimamiwa vizuri pato lake litaingia kwenye familia na kuweza kuendesha
maisha yao ya kila siku badala ya jasho hilo kufaidiwa na watu wengine.
Kwa upande mwingine alisema msiba wa
Knii huyo
alivyoweza kuitangaza Tanzania kupitianumba ni pigo kwa tasnia ya filamu kutokana na namna msaa kazi zake.
Mwakifamba alisema TAFF itamkumbuka kwa
mambo mengi,kwani mbali na kuwa mwanachama kupitia chama cha Waigizaji
Kinondoni,pia alikuwa mjumbe wa kamati ya TAFF ya kuandaa mapendekezo ya
marekebisho kanuni ya sheria za filamu za mwaka 2011.
Vilevile Kanumba alikuwa ni mmojawapo ya
wafadhili wa Shirikisho hilo na alikuwa na mchango mkubwa katika kuleta
umoja na mapinduzi ya kweli katika tasnia ya filamu.