Monday, April 9, 2012

MACHANGUDOA WAOMBA WAACHIWE HURU JIJINI DAR

BAADHI ya machangudoa wanaoshi katika mtaa wa Madenge kata ya buguruni wameomba waachiwe huru ili waweze kuendelea na biashara yao ambayo ndiyo inayowaingizia kipato.

Waliyasema hayo mapema leo hii baada ya kikundi kilichoibuka na kujiita chui walinzi shirikishi kutoka msikitini wanaowanyanyasa na kuwazuioa wateja wasiingie kwenye nyumba zao.

Wilimina Elifas ni mmoja wa kinadada wanaofanya biashara hiyo na alisema kuwa anaiomba serikali itambue uwepo wao kwani hata viongozi wa serikali wanakwenda kupata huduma mahali hapo.

"Serikali inajua kabisa kwamba biashara hii ipo kwanini isituachie hata na sisi tulipe kodi? mbona viongozi wa serikali tena wajuu kabisa wanakujaga hapa kupata huduma?hii ndio bihashara pekee inayotuingizia kipato cha kuwezesha familia zetu", alisema Willimina.

Nao kinadada wengine walionyesha kutaka kuachwa waendelee na biashara yao kwani ndiyo biashara pekee inayo wawezesha.

No comments:

Post a Comment