Wednesday, April 11, 2012

JEHI LA POLISI DAR LAINGIA DOA

JESHI la polisi Mkoa wa Dar es Salaam limejikuta likiingia doa baada ya kuwavamia na kuwapiga mabomu waumini wa kanisa la Efatha wakiwa ibadani Tarehe 9 Aprili jumatatu ya Pasaka.

Akizungumza na waandishi wa habari leo hii Mchungaji msaidizi wa kanisa hilo, Godson Mmari alisema kuwa, siku hiyo wakati ibada ikiendelea, wakiongozwa na Mchungaji David Mwakisole ghafla waliona waumini wamevamiwa na watu ambao walitambuliwa kuwa ni Polisi.

Mmari alisema kuwa,Polisi hao walitupa mabomu hayo ya machozi  ndani ya kanisa kuelekea Madhabauni na kuelekea kwa waumini walikokua katika ibada.

Alisema kuwa polisi hao waliingia kanisani hapo kwa kuvunja na kuruka ukuta kwani walikuta kanisa limezungushiwa ukuta pande zote nne na mageti yalikuwa yamefungwa.

"Walikuta mageti yamefungwa wakaamua kuvunja na kuruka ukuta wakati sisi tukiwa tunaendelea na ibada", alisema Mchungaji huyo kwa machungu.

Aliendelea kusema kuwa wanafahamu kuwa kitendo cha polisi kuvamia na kuvuruga ibada ni kinyume na sheria na katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania iliyowekwa huru na kuabudu na sheria za nchi zinazoeleza kwamba ibada ziheshimiwe.

"Kulikuwa na tatizo gani polisi wasisubiri nje ibada iishe na wachukue watu wanaotaka kuwachukua?", aliongeza.

Naye Katibu mkuu wa Efatha Foundation Nattu Shilla, alisema kuwa kuhusu sababu za wao kuvamiwa ni kwamba wanadhaniwa kuwa si wamiliki halali wa Kiwanja walichopo hivi sasa amba cho kinatajwa kuwa ni kiwanja namba 90 eneo la Mwenge Nuru Centre.

Shilla alisema, kuhusu umiliki wa eneo hilo kuwa wao ndio wamiliki halali wa Eneo hilo na vielelezo vyote vya umiliki wa eneo hilo wanavyo.

"Nivyema ieleweke kuwa,Efatha Foundation LTD  iliponunua eneo hili tamani yake ilijumuisha majengo yaliyokuwa yamejengwa huma ana Mangula Mechanical and Machine tools iliyo filisika", alisema Shilla.