Tuesday, April 9, 2013

WEZI SUGU WA VIPURI WAKAMATWA MKOANI ARUSHA

DSC02243Watuhumiwa wa sugu wa wizi wa mafuta na vipuri katika minara mbalimbali ya simu hapa nchini wakiwa chini ya ulinzi wa jeshi la polisi muda mfupi baada ya kukamatwa wakijaribu kufanya uhalifu katika mnara uliopo eneo la Tengeru jana,kulia ni Njamas Lyoka(27) na mwenzake,Essau Bussa(44).
……………………………………………………………….
Na Gladness Mushi wa Fullshangwe-Arusha
VINARA sugu   ambao hujihusisha na wizi wa vipuri na mafuta ya
Transformer  katika minara mbalimbali hapa nchini  wanashikiliwa na

jeshi la polisi mkoani Arusha baada ya kukamatwa muda mfupi kabla ya

kutaka kuiba vipuri katika mnara wa Tengeru.
Wizi hao walifanikiwa kukamatwa baada ya taarifa za wao kutaka kuvamia
katika mnara huo na kuiba kubainika na hivyo kuwekewa mtego maalum wa

jeshi la polisi kwa kushirikiana na viongozi wa kampuni ya Northen

Engineering na kampuni ya Ulinzi ya Security [Intelligence]na

kukamatwa.
Kampuni hizo mbili ndizo zinajishughulisha kuhudumia minara hiyo ya
simu katika mikoa 14 ya minara  hapa nchini na hivyo kila mara

kulazimika kulipa fidia kwa wizi unaofanyika katika minara hiyo kutoka

kwa makampuni ya simu wanaomiliki minara hiyo.
Akuiongea mara jana kwa njia ya simu mkuu wa kituo cha polisi Tengeru
[OCS]Deusi Masala alisema watuhumiwa hao wawili wanaendelea

kushikiliwa na jeshi la polisi katika kituo hicho kwa mahojiano na

watafikishwa mahakamani siku ya jumatatu[leo].
Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Njamas Liyoka [27] mkazi wa sakina
Arusha na Esau Busa [44] mkazi wa Mbauda ambae huishi jijini Dar es

salaam ambao wamefunguliwa hati ya mashtaka namba Teng/Rb 317/2013.
Nae msemaji wa kampuni ya Ulinzi ya Inteligence Security Nasoro
Shabani akiongelea tukio hilo alisema wamefarijika kukamatwa kwa watu

hao ambao wamekua wakiwasababishia hasara kubwa ambayo hutokana na

ulipaji wa fidia pindi wizi unapotokea.
‘’Siosi kama kampuni leo tunaona tumepata mwanga juu ya wizi
wanaotufanya tupate hasara ya fedha kila mara kwa kulipa fidia

kutokana na upotevu wa mafuta na vipuri katika minara mbalimbali hapa

nchini’’alisema Nasoro.

No comments:

Post a Comment