Tuesday, April 9, 2013

SUMATRA YAKABIDHI KWA JESHI LA POLISI VIFAA VYA KUPIMA KILEVI KWA AJILI YA KUWABAINI MADEREVA WA MABASI NA MALORI WALEVI


Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri 
wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), Ahmad Kilima 
(kulia), akimkabidhi Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini
 (IGP), Said Mwema, vifaa maalumu vya kupima 
ulevi vyenye thamani ya sh.milioni 13 
vilivyotolewa na Sumatara kuwabaini madereva 
walevi katika hafla iliyofanyika Makao 
Makuu ya Sumatra Dar es Salaam leo. Kushoto 
ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini,
 Mohamed Mpinga.
 Maofisa wa Jeshi la Polisi waliokuwepo kwenye hafla hiyo. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Polisi Jamii Nchini Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP), Lazaro Mambosasa, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Mkoa wa Kiposi wa Kinondoni (SSP), Ibrahim Mwamakula, Mkuu wa Trafiki Kanda ya Maalumu ya Dar es Salaam (ACP), Salehe Mmbaga na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Amiri Juma Konja kutoka Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.
 Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa 
kwenye hafla hiyo.
 Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Polisi Jamii Nchini 
Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP), 
Lazaro Mambosasa,
 Maofisa hao wa polisi wakiwa kwenye hafla hiyo.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Said Mwema, 
akihutubia kwenye hafla hiyo.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Said Mwema (wa pili kushoto), akiwa na viongozi wenzake. Kutoka kulia Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Amiri Juma Konja kutoka Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Mohamed Mpinga, Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), Ahmad Kilima na Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini, Advera Senso.
 Viongozi hao wakifurahi baada ya makabidhiano ya vifaa hivyo.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Said Mwema (katikati), akimkabidhi vifaa hivyo Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabara Nchini, Mohamed Mpinga. Anayeshuhudia kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Sumatra, Ahmadi Kilima.
 IGP Said Mwema akiwaongoza wageni waalikwa na 
waandishi wa habari kupasha ikiwa ni kujipongeza baada ya kupokea vifaa hivyo. 
(Picha habari na habari za jamii blog)
 Wafanyakazi wa Sumatra, Askari Polisi na wageni waalikwa na waandishi wa habari wakiwa kwenye shughuli hiyo.
IGP Said Mwema (kushoto), akiteta jambo na Kaimu Mkurugenzi wa Sumatra, Ahmadi Kilima baada ya kupokea vifaa hivyo. Kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini Mohamed Mpinga.

 Na Dotto Mwaibale

MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra), imetangaza kiama kwa madereva walevi baada ya kulikabidhi Jeshi la Polisi vifaa maalumu vya kupima ulevi.

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya vifaa hivyo Dar es Salaam leo kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Said Mwema, Kaimu Mkurugenzi wa Sumatra, Ahmad Kilima  alisema hawatakauwa na huruma kwa dereva yoyote atakayebainika akiendesha gari akiwa amelewa.

"Hatutakuwa na huruma na dereva atakayaebainika akiendesha gari linalofanya kazi chini yetu huku akiwa amelewa kwani tutamfutia leseni yake na hata fanyakazi hiyo tena hapa nchini" alisema Kilima.

Alisema dereva atakayefutiwa leseni yake hata wezakukimbilia kuendesha chombo kingine chochote cha moto kinachofanya kazi chini ya Sumatra iwe gari kubwa, basi, meli, Treni na ndege.

Alisema hapa nchini kumekuwa na matatizo makubwa ya ajali za barabarani kutokana na miundombinu ya barabara kuwa mibovu, magari machakavu, mabasi kutengenezwa kwa chesesi ya magari makubwa na mambo mengine mengi ikiwemo ya madereva kuendesha wakiwa wamelewa.

Alisema asilimia 76 ya ajali zimekuwa zikisababishwa na wanadamu na hasa madereva wazembe, asilimia 16 magari machakavu na asilimia 8 uchakavu wa barabara.

Alisema Sumtra kwa upande wake imejipanga kuhakikisha ajali hizo zinapungua au kwisha kutokana na jitihada inayozifanya kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi.

Kilima alisema vifaa walivyocvikabaidhi jeshi hilo vinathamani ya sh.milioni 13 na kwa kuanzia vitatumika kuwapimia madereva 2000 na kuwa Sumatra itakuwa ikiviongeza kadri vitakavyokuwa vikipatika.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Said Mwema alisema polisi imejipanga vilivyo katika kupambana na uhalifu wa barabarani kwa kushirikiana na Sumatra na kuwa vifaa hivyo walivyokabidhiwa ni hatua nyingine ya mafanikio katika kukabiliana na tatizo la ajali hapa nchini.

Alisema vifaa hivyo vitawasaidia watanzania milioni 44 wanaotumia barabara na kuboresha mpango mzima wa jeshi la polisi katika ufanyaji wa kazi zake.

"Kazi kubwa ya jeshi la polisi ni kubaini lilipo kosa, kuzuia na na kudhibiti hivyo vifaa hivi vitatuongezea kasi ya utendaji kazi zetu za kudhibiti uhalifu" alisema Mwema.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Polisi Jamii Nchini, Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi (SSP), Lazaro Mambosasa aliitaka jamii kubadilika na kufuata sheria bila ya shurti na kuacha vitendo vya uhalaifu.

Katika hafla hiyo viongozi mbalimbali wa jeshi hilo na wa Sumatra walihudhuria na wadau wa sekta ya usafirishaji.

No comments:

Post a Comment