Wanafunzi wa shule mbalimbali za sekondari jijini Dar zikiwemo Makongo,
Airwing, Mtakuja Beach na Chang'ombe wakiwa Safarini Kulekea katika
ziara ya kutembelea Magofu ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara ambayo yapo
kwenye orodha ya urithi wa Dunia katika safari ya iliyoandaliwa na
Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) wakati wa kumbukumbu ya
Biashara ya Utumwa na kuwaenzi waliopoteza maisha katika biashara hiyo
iliyokuwa imeshamiri katika maeneo hayo.
Biashara hiyo ya Watumwa ilifanyika kwa miaka 400 na kuhusisha zaidi ya
Waafrika milioni 15 na watu wenye asili ya Afrika ambao walikuwa
waathirika wa ukatili wa Utumwa na kuendelea kuteseka na madhara yaa
biashara ya Utumwa.
(Picha na Mo Blog.)
Kiongozi wa msafara huo Afisa Habari wa ngazi ya kimataifa Kitengo cha
Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Stella Vuzo (wa tatu kushoto)
njiani kuelekea Kilwa Kisiwani.
Afisa Habari wa ngazi ya kimataifa Kitengo cha Habari cha Umoja wa
Mataifa (UNIC) Bi. Stella Vuzo akitoa mwongozo wa ziara kwa wanafunzi
baada ya kufika katika bandari ya Kilwa kabla ya kuelekea Kilwa Kisiwani
kwa ziara ya mafunzo ya kumbukumbu za biashara ya Utumwa.
Ambapo alisema lengo la ziara hiyo ni kutaka Wanafunzi kujifunza
madhara ya biashara ya Utumwa jinsi ilivyofanyika na madhara yake na ili
waweze kusaidia katika jitihada za kuitokomeza biashara hiyo ambayo
mpaka sasa bado inaendelea kufanyika kimya kimya katika maeneo
mbalimbali nchini na kuwataka kuzijua haki zao za kibinadamu na
kutogeuzwa bidhaa za kuuzwa kutoka sehemu moja kwenda nyingine kwa
udanganyifu wa kupelekwa kufanya kazi nchini za kigeni.
Mwl. Mwasi wa shule ya Sekondari Chang'ombe (mwenye nyekundu) akiwa ndani ya boti na wanafunzi kuelekea Kilwa Kisiwani.
Wanafunzi wakiwasili Kilwa Kisiwani.
Picha juu na chini' Tour Giude' Dullah akitoa malekezo ya ramani ya
sehemu watakazotembelea wanafunzi hao ili kupata ufajamu wa jinsi
Historia ya eneo hilo ilivyokuwa hadi kufikia biashara ya Utumwa na
majengo yaliyokuwa yakitumika Karne ya 9 baada ya kuzaliwa Kristo.
Wanafunzi wakichukua maelezo muhimu kutoka kwa Mtaalamu wa masuala ya
Historia ya Asali ya Kilwa Kiswani na Songo Mnara wakiwa kwenye makaburi
waliyozikwa viongozi waliotawala eneo la Kilwa Kisiwani.
'Tour Giude' Dullah akiendelea kutoa ufafanuzi wa maeneo mbalimbali
yaliyotumika enzi za biashara ya Utumwa ikiwemo Misikiti, Gereza na
Nyumba ya Sultan Hassan Bin Sultan ambaye alikuwa mtawala wa eneo hilo.
Wanafunzi wakielekea kwenye Gereza maarufu lililokuwa likitumiwa na kufunga watumwa.
Muonekano wa Gereza hilo kwa Nje Lango Kuu la kuingia.
Mhifadhi Mambo ya Kale Kilwa Kisiwani Yussuph Bakari Said (mwenye shati
la zambarau) akionyesha Kisima kilichokuwa kikitumiwa na wafungwa ndani
ya Gereza hilo.
Wanafunzi wakiangalia Kisima kimoja wapo ndani Msikiti wakati huo.
Mmoja ya wananfunzi wa shule hizo walioitembelea maeneo hayo ya
kumbukumbu akishangaa Mzinga uliodumu mpaka leo toka Karne ya 9 baada ya
kuzaliwa Kristo.
Mafunzo yakiendelea kutolewa kwa wanafunzi hao.
Moja ya Majengo ya Nyumba ya Sultan Hassan Bin Sultan aliyeoa wanawake 77 enzi za utawala wake.
Mhifadhi Mambo ya Kale Kilwa Kisiwani Yussuph Bakari Said katika picha
ya kumbukumbu na Afisa Habari wa ngazi ya kimataifa Kitengo cha Habari
cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Stella Vuzo aliyeambatana na Phillip
Musiba pamoja na wanafunzi wa shule mbalimbali za jijini Dar es Salaam
katika siku ya kuwakumbuka wahanga wa biashara ya Utumwa.
Wanafunzi wakisindikizwa na Afisa Habari wa ngazi ya kimataifa Kitengo
cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Stella Vuzo (mwenye kitenge)
kupanda boti kurudi Bandarini baada ya kuhitimisha ziara yao Kilwa
Kiswani.
Afisa Habari wa ngazi ya kimataifa Kitengo cha Habari cha Umoja wa
Mataifa (UNIC) Bi. Stella Vuzo aliyeambatana na mfanyakazi mwenzake
Phillip Musiba, walimu waliojumuika na wanafunzi wa Shule ya Sekondari
Kilwa katika ziara hiyo katika picha ya pamoja.
No comments:
Post a Comment