Monday, April 8, 2013

CWT YWATAKA WALIMU, WAZAZI NA BUNGE KUUNGANA KUILAZIMISHA SERIKALI KUONGEZA MISHAHARA YA WALIMU

Rais wa Chama sha Walimu Tanzania CWT akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) leo katika makao akuu ya Chama hicho.


Chama Cha Walimu  Tanzania (CWT) kimewataka walimu wote Tanzania, Bunge la Tanzania pamoja na wazazi wa Wanafunzi  kuungana kwa pamoja,   kuilazimisha Serikali kukubali kukaa meza moja na CWT  kujadili mishahara pamoa na Posho za Walimu kwa ajili ya Mwaka ujao wa Fedha.

Rais wa CWT Bw, Gratian Mukoba, ameyasema hayo leo katika mkutano wake  na waandishi wa habari uliofanyika katika makao makuu ya Chama hicho jijini Dar es Salam.

Bw , Mukoba amesema kuwa chama kimefikia uamuzi huo wa kuwashirikisha walimu wote pamoja na wazazi na Bunge baada ya Serikali kukataa kurudi mezani kujadiliana na CWT Kuhusu  mishahara na posho za walimu wa Mwaka wa Fedha wa 2013/2014.

Amesema kuwa, baada ya Mahakama kuamuru  CWT  kurudi  Mezani kwenye hukumu  ya tarehe 02 Agosti 2012, CWT iliandika barua  kuieleza serikali kuwa chama kipo tayari kukutana  kwa ajili ya  Majadiliano, lakini Mh Philip Mulugo Naibu waziri wa Elimu aliagiza hoja za kujadiliwa  katika kikao hicho kuwa ni  hoja  zilizo sababisha walimu kugoma, jambo ambalo CWT kilipinga, kwa maelezo kuwa Serikali haikuwa na nia thabitiya kujadiliana na CWT.

“Serikali na CWT, ilikutana tarehe  09 januari 2013 kwenye Baraza a Majadiliano na walimu ambapo CWT Kilikubaliana na  hoja ya Serikali kufanya Majadiliano japokuwa CWT, Tangu mwanzo hakikuona nia thabiti ya serikali kujadilana ambapo CWT kilitakiwa kuandaa hoja yake ya kuwasilisha kabla ya majadiliano kuanza,ambapo chama kiiwasilisha lakini Serikali ilishindwa kutoa Majibu”, amesema Mukoba.

Ameongeza kuwa Serikali iliweka msimamo wake wa kutokujadili  mishahara ya walimu baada ya Makatibu wakuu wa TALGWU, TUGHE, CWT, na TUCTA kukutana na Katibu mkuu kiongozi Ikulu jijini Dar es Salaa, katika kikao cha Tarehe 02 Aprili, 2013 kilichohudhuriwa na Makatibu wakuu wa Utumishi, TAMISEMI.

Aidha CWT kimetaka wito huo kuzingatiwa kuhakikisha kuwa Maslahi ya walimu, yanapatikana ili kuepusha Mgogoro unaoweza kujitokeza ikiwa Serikali itaamua kujipangia Mishahara ya Walimu bila kujadiliana na CWT.

Nasisitiza Jamani tuungane Walimu na wazazi kutetea Maslahi ya walimu kuepusha mgogoro utakaosababisha wanafunzi milioni 10 kukosa masomo ikiwa walimu watagoma.

No comments:

Post a Comment