Monday, April 8, 2013

HAYA NDIYO MAAZIMIO NANE YA KAMATI KUU YA CHADEMA

Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CHADEMA Mhe. John Mnyika alizungumaza na Waandishi wa Habari kuhusu maazimio na maamuzi mbalimbali ya Kamati Kuu iliyokutana tarehe 03-05/04/2013 katika Hoteli ya Blue Pearl Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.
Aliyataja masuala nane yaliyomo katika agenda moja ya “Taarifa ya Hali ya Siasa”


  1. Matukio yaliyotokea Bungeni mwezi Februari 2013 na yatokananayo
  2. Masuala yanayohusu Madiwani wa CHADEMA
  3. Kutekwa na kuteswa na Absalom Kibanda na Dk Ulimboka Steven
  4. Vurugu za Kidini na kujeruhiwa na kuuawa kwa baadhi ya viongozi wa dini
  5. Kupigwa kwa wanachama wa CHADEMA Dodoma alikohusika Ismail Aden Rage (Mbunge) na matukio yafananayo
  6. Hali tete katika kijiji cha Ruaha - Kilosa na Masasi - Mtwara
  7. Ziara ya rais wa China na usiri wa mikataba 17 ambayo ni haki ya mwananchi kufahamu kilichomo
  8. Maafa ya kuporomoka kwa mwamba Arusha, na jengo Dar es Salaam kunakotokana na uzembe

No comments:

Post a Comment