Thursday, April 18, 2013

SUMATRA YAADHIBU DALADALA 144 KWA MAKOSA MBALIMBALI JIJINI DAR ES SALAAM


 

dala

 MAMLAKA ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), imekamata magari 144 ya abiria kutokana na kufanya makosa mbalimbali.
Akizungumza na wandishi wa habari  jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Mfawidhi Kanda ya Mashariki wa Sumatra, Conrad Shiyo, alisema magari hayo yamekamatwa kuanzia mwanzoni mwa wiki hii.
 Alisema kati ya magari hayo 63 yaliokamatwa ni kutokana na makosa ya kuwatoza abiria nauli kinyume na ile elekezi,  kutumia tiketi za zamani na kukatisha njia huku wakijua fika kuwa kufanya hivyo ni kosa.
 “Tumegawa chati za bei kuanzia Jumatatu kwa kila gari, zenye utambuzi wa bei ya nauli za zamani na mpya hivyo kila mwananchi anayo haki ya kuoneshwa chati hiyo pindi anapotaka na akinyimwa kuiona hilo ni kosa na mhusika atachukuliwa hatua,”alisema Shio.
 Aliyataja makosa mengine kuwa ni pamoja na magari 71 ambayo madereva na makondakta wake walikutwa wakiwa hawakuvaa sare za kazi na matumizi ya lugha chafu kwa abiria ambako adhabu za makosa hayo faini zake zinaanzia sh 100,000 na kuendelea.
 “Nawashukuru wananchi kwa ushirikiano wao katika kufanikisha operesheni hii  ya kukamata magari haya, tunawaomba waendelee kutuletea taarifa za madereva hao ili tuweze kuwashinda wakorofi hawa wasiotaka kutii sheria za nchi”alisema Shio.

No comments:

Post a Comment