Thursday, April 18, 2013

Hospitali ya taifa ya Muhimbili yaadhimisha miaka 13 huku ikikabiliwa na changamoto tele.


Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali wa Serikali, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Donald Mmbando akitoa hotuba ya Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mh. Dk. Hussein Mwinyi wakati wa kufungua rasmi maonyesho ya huduma za hospitali ya taifa ya Muhimbili katika kuadhimisha miaka 13 ambapo amezungumzia nia ya serikali kusaidiana na hospitali hiyo katika kutafutia ufumbuzi changamoto zinazoikabili ili iweze kuendelea kutoa huduma kwa wananchi katika kiwango cha juu kama ilivyokusudiwa.
Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali wa Serikali, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Donald Mmbando (katikati waliokaa)katika picha ya pamoja na wakuu wa idara mbalimbali na wajumbe wa bodi ya wadhamani mara baada ya kufungua rasmi maonyesho ya huduma za hospitali ya taifa ya Muhimbili katika kuadhimisha miaka 13 na miaka mitatu kama hospitali ya ubingwa wa Juu ya taifa.

*******
Serikali ya Tanzania imepongezwa kwa juhudi zake ilizofanya na inazoendelea kufanya kwa sasa katika kuhakikisha kwamba majukumu makubwa matatu ya Hospitali ya taifa ya Muhimbili yanatekelezwa ipasavyo.
Pongezi hizo zimetolewa wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya huduma za hospitali ya taifa ya Muhimbili katika kuadhimisha miaka 13 kama hospitali ya taifa na miaka mitatu kama hospitali ya ubingwa wa juu ya taifa uliofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Taarifa ya hospitali hiyo imesema kwa upande wa tiba imefanikiwa kuongeza idadi ya vitanda kuwa 1271, na kuongeza idara na kuwa 30.

No comments:

Post a Comment