Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Prof. John Nkoma akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutoa tamko la pamoja
kwa umma la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania na Makampuni yanayotoa
Huduma za Simu kuhusu Usajili wa namba za Simu za Mkononi Tanzania
ambapo amesema Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ikishirikiana na
makampuni ya Simu na vyombo vya usalama imeanza kampeni endelevu yenye
lengo la kuwabaini wote wanaohusika na uvunjifu wa sheria ili kuwalinda
watumiaji wema na jamii kwa ujumla kwa ajili ya kuimarisha usalama na
kuleta maendeleo na ustawi wa wananchi.
Mkurugenzi
Mkuu wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo Tanzania Diego Gutierrez
akielezea jinsi kampuni yake ilivyojidhatiti katika kutoa huduma kwa
wateja na kuhakikisha kila namba ya simu inayotolewa na kampuni ya simu
ya Tigo inasajiliwa kwa mujibu wa kifungu cha 102 (1) cha Sheria ya
mawasiliano ya Elektroniki na Posta (EPOCA).
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Prof. John Nkoma (wa
tatu kushoto) akiwa meza kuu na Wakurugenzi Watendaji Wakuu wa Kampuni
yanayotoa huduma za simu nchini.
Baadhi maafisa mbalimbali na wawakilishi wa makampuni yanayotoa huduma za simu nchini katika mkutano huo.
Sehemu ya wawakilishi mbalimbali wa vyombo vya habari nchini.
No comments:
Post a Comment