Sunday, April 14, 2013

Push Mobile kutoa ving’amuzi 91 katika promosheni ya Kidigitali Zaidi



Na Mwandishi wetu
Kampuni  ya Push Media Mobile imetoa ving’amuzi  91 kwa ajili ya kushindaniwa  katika promosheni ya “Kidigitali Zaidi”  ambayo lengo lake kubwa ni kuongeza idadi ya watumiaji wa mfumo wa matangaza ya televisheni ya kidigitali.
Meneja Masoko wa Push Media Mobile, Rugambo Rodney (pichani), amesema  kuwa promosheni hiyo itaanza kwanza kwa miezi mitatu ambapo kila siku mshindi mmoja atajishindia king’amuzi.
Rugambo alisema kuwa ili kushinda king’amuzi  tuma neno “shinda” kwenda namba 15522 na mshindi anaweza kujipatia king’amuzi cha aina ya StarTimes, DiGi Tek au Zuku.
Alisema kuwa wamesikia kilio cha watanzania kuhusiana na gharama za kupata king’amuzi na wao kuanzisha promosheni hiyo ambayo washindani watapata king’amuzi sawa na ‘bure’ na kuzishukuru kampuni za Global Publishers, Kituo cha televisheni cha DTV, Times FM, Magic FM, Maisha Club na Baakubwa kwa ushirika wao katika kampeni hiyo.
Kwa mujibu wa Rugambo, promosheni hiyo ni endelevu na lengo lao ni kuona watanzania wanapata haki ya kupata habari kwa njia ya televisheni.
“Tumejiandaa vilivyo kwa ajili ya promosheni hii, kila siku kumekuwa na kilio cha watanzania kuhusiana na gharama za kupata king’amuzi, wengi hawana na wanakosa taarifa za kila siku ikiwa pamoja na habari za michezo, sanaa, urembo na za kisiasa,” alisema Rugambo.
Alisema kuwa jumla ya shs  25 millioni zitatumika katika  promosheni hiyo ambapo mshindi wa siku ya 90 atapata king’amuzi na televisheni bapa ‘flat screen’ yenye thamani ya sh. 1 million.

No comments:

Post a Comment