JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
14 Aprili, 2013
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)
linasikitika kutangaza kifo cha Meja Jenerali Rashid Mnalihinga Makame
(mstaafu) ambaye amefariki dunia tarehe 14 Aprili, 2013 saa kumi na mbili na nusu asubuhi, katika
Hosptali ya TMJ.
Pamoja na nyadhifa mbalimbali alizowahi kushika
Jeshini na Serikalini, Meja Jenerali Rashid Mnalihinga Makame (mstaafu) alikuwa
Mkuu wa JKT wa tano. Kama mnavyofahamu umuhimu wa JKT, yeye ni miongoni mwa
Makamanda walioleta tija kubwa katika kuwalea Vijana wa Kitanzania na
kuwajengea nidhamu na uzalendo.
Mpango wa Mazishi unafanywa, mtajulishwa baadae juu ya
wapi na lini atazikwa Meja Jenerali Rashidi Mnalihinga Makame (Mstaafu). Msiba
upo nyumbani kwake Mikocheni, karibu na nyumbani kwa Hayati Mwl J.K Nyerere.
MUNGU
AILAZE MAHALI PEMA PEPONI
ROHO YA
MAREHEMU
Meja Jenerali Rashidi Mnalihinga Makame (MSTAAFU) AMINA.
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
SLP 9203, Simu: 0764-742161
Email:ulinzimagazine@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment