Na Bryceson Mathias
Nianze
kwa kusema hivi Bundi aliyeiandama Imani ya Madhebu yetu kwa lengo tu
la kuboresha maslahi ya mtu aliyeasisi hoja ya kuchinja ili watanzania
waingie katika malumbano, sasa afahamu hoja yake ya uchovu imeshindwa.
Haiingii
akilini kwa mtu anayetegemewa, mwenye nafasi na dhamana kubwa
iliyotukukuka, iwe ki-Imani au Ki-Itikadi, kuibua migogoro ya dini
mithili ya David na Mary katika kitabu cha Kingereza tulivyosoma hapo
kale kidogo, walivyogombea Mtoto na kumvuta mikono hadi ikakatika.
Kwa
muda mrefu nimekuwa nikisikiliza na kusoma malumbano ya kuchinja
nikabaini katika suala la hilo mmoja wetu miongoni mwa pande
zinazobishishania uhalali huo; anavutia kamba upande wakebadala ya kukaa
meza moja na kutengeneza maridhiano.
Kilichopelekea
mgogoro huu hasa, yawezekana kabisa umetokana na kupotoka kwa baadhi ya
dni ambazo pengine zinajiona ni bora kuliko Dini nyingine, huku
wakisahau kujali kwamba wenzao wenye miiko ya dini zao ya kutokula
kitoweo kilichochinjwa au kutochinjwa na dini nyingine.
Kwa
mfano; kwa mila na desturi katika Jamii au familia, kuna watu hawali
vitu fulani fulani kama Njiwa, Kuku, Bata, Nyama, Samaki na vitu vingine
katika koo na familia zao. Hivyo hatupaswi kuwalazimisha au kuwapuuza
kwa kile wanachokiamini, na akitokea mtu wa namna hiyo atakuwa Mkorofi.
Kimsingi
kwa ukweli halisi, Serikali haitakiwi kubabaika kiasi cha kuuma maneno
na kukaa kimya, bali isema wazi kwamba kila mtu anaweza kuchinja
kutokana na imani yake ilimradi tu havunji sheria za nchi kwa maadili
yoyote.
Je;
mtu akila Mlenda nyumbani kwake au akaamua kuchinja Kuku, Bata, Njiwa,
Mbuzi au kitoweo chochote alichonato, kuna ulazima wa kumlazimisha
achinjiwe? Je tuna haja ya kumlalamikia na kumtuhumu kiasi cha
kumsababishia ghasia na magombano akiwa ametulia kwake?


Lakini
nakubaliana kwamba, Mfanya Biashara wa Kikristo au Wa K-Islamu, akitaka
kufanya Biashara ya Nyama, Sherehe, Msiba, au kusanyiko lolote
linalohusisha Kula, ni lazima uchinjaji wa kitoweo chake uhusisishe
ridhaa ya uchinjaji ambao utaruhusu Watu wote kwenye kusanyiko hilo
kula.
Kwa
maana hiyo viongozi, wananchi na waumini wa madhehebu mbalimbali nchini
waelewe kwamba, Wapagani, Wakristo, Wa-Islamu wanaweza kuchinja kitoweo
chao na wakala endapo wako katika familia zao, kama ilivyokuwa
ikifanyika hapo awali bila kuathiri chochote ili mradi havunji sheria za
nchi.
Hivi
kama huli kitu, na wengne wanakula, kwa nini upate uchoyo na uroho wa
kutaka kula kwa tamaa yako? Mimi sioni kitu hapa maana hakuna Mkristo au
M-Islam ambaye ni bora kuliko mtu wa Dini zingine, hiyo inatokana na
miiko au mila za dini zao za kutokula vitoweo vilivyochinjwa na dini
nyingine.
Mbona
huko Ulaya, wenzetu wana maduka ya Bucha ambapo Wakristo wana ya kwao
wananunua wanachokita na wa- Islamu wana ya kwao wanunua wanachokita kwa
nini sisi tugombane hata kwa vitu ambavyo hatuvili? ningekuwa mimi,
akichinja Mu-Isalmu nakula; maana najua jinsi ya kufanya ili nile
Hivyo Usichokula usikionee uroho na tamaa ya kukila, na pia tusiwabeze wanaokula.
No comments:
Post a Comment