Kituo
cha televisheni cha SuperSport cha Afrika Kusini kitaonesha moja kwa
moja mechi sita za Ligi Kuu ya Vodacom katika Super Week kati ya Aprili
11 na Mei 18 mwaka huu.
Mechi
hizo ni kati Azam na African Lyon itakayochezwa Aprili 11 mwaka huu
badala ya Aprili 10 mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam Complex ulioko
Chamazi, Dar es Salaam. Yanga na Oljoro JKT ambayo sasa itachezwa Aprili
13 mwaka huu badala ya Aprili 10 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Azam
na Simba itakayochezwa Aprili 14 mwaka huu badala ya Aprili 13 mwaka
huu Uwanja wa Taifa, na mechi kati ya Coastal Union na JKT Ruvu
itakayochezwa Aprili 16 mwaka huu badala ya Aprili 10 mwaka huu.
Mechi
nyingine ya Super Week itakayochezwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga
ni kati ya Mgambo Shooting na Yanga itakayofanyika Aprili 17 mwaka huu
badala ya Aprili 13 mwaka huu.
Pia
mechi nyingine itakayooneshwa live na SuperSport ni kati ya Yanga na
Simba itakayofanyika Mei 18 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Kutokana
na mechi za Super Week, mechi kati ya Mtibwa Sugar na Oljoro JKT
iliyokuwa ichezwe Aprili 13 mwaka huu sasa itachezwa Aprili 17 mwaka huu
Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro.
TFF YATAKA MAELEZO YA MCHEZAJI KUHUSU RUSHWA
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemtaka mshambuliaji Nsa Job wa
Coastal Union kuwasilisha maelezo yake juu ya madai kuwa alipewa rushwa
ya sh. milioni mbili ili asiifunge moja ya timu vigogo vya soka nchini.
Job
alikaririwa Aprili 3 mwaka huu na kituo cha redio cha Clouds FM katika
kipindi cha Amplifier kuwa alipewa kiasi hicho cha fedha na kiongozi wa
timu husika ili asiifunge katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom, lakini
alipokea fedha hizo na kuifunga timu hiyo.
Baadaye
kiongozi huyo alikuwa akimtaka arejeshe fedha hizo. Pia TFF
imekiandikia kituo hicho cha redio kutaka nakala ya kipindi hicho ili
pamoja na maelezo ya mshambuliaji huyo vipelekwe katika Kamati ya
Nidhamu kwa ajili ya hatua za kinidhamu.
TFF
itachukua hatua kali dhidi ya Job iwapo hatawasilisha maelezo yake
kuhusiana na suala hilo, na imetaka wadau kutoa ushirikiano ili iweze
kupambana kikamilifu na vitendo vya rushwa kwenye mpira wa miguu.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment