Maandamano ya raia wa Rwanda wanaoishi nchini Tanzania pamoja na
wanafunzi wa shule mbalimbali za jijini Dar es Salaam wakijipanga katika
ukumbi wa New World Cinema tayari kuanza maandamano ya kuadhimisha
miaka 19 ya mauaji ya Kimbari ya Rwanda kuelekea ukumbi wa mikutano wa
Mlimani City.
(Picha na Zainul Mzige wa Mo Blog)
Picha juu na chini Umati wa maandamano yakielekea katika ukumbi huo.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo Dr. Salim Ahmed Salim njiani kuelekea kwenye ukumbi wa mikutano Mlimani City.
Mgeni rasmi Dr. Salim Ahmed Salim (wa tatu kulia) akiwa na balozi wa
Rwanda nchini Tanzania Mh. Benjamin Ruganganzi (wa tatu kushoto)
wakisubiri kupokea maandamo ya maadhimisho ya miaka 19 ya mauaji ya
Kimbari ya Rwanda katika viwanja vya Mlimani City jijini Dar.
Mgeni rasmi katika maadhimisho ya 19 ya mauaji ya Kimbari ya Rwanda Dr.
Salim Ahmed Salim akizungumzia kumbukumbu ya mauaji hayo ambapo amesema
historia ipo kwa ajili yetu sote kujikumbusha yaliyopita ili tuweze
kupanga yajayo na kuwa mauaji ya Kimbari ni mzigo wetu sote na tunapaswa
kujifunza kutambua alama za watu wa jamii moja kuanza kuhitilafiana na
kutafuta namna ya kuzitatua kabla hazijaleta athari.
Na pia alichukua fursa hiyo na kunukuu maneno yaliyowahi kusemwa na
Baba wa Taifa wa Tanzania Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere " Ukweli
ni kwamba kila sehemu ya Afrika ina ihitaji Afrika kwa pamoja na Afrika
kama bara inahitaji kila sehemu ya bara la Afrika".
MC katika maadhimisho ya miaka 19 ya mauaji ya Kimbari Usia Nkhoma
akirekebisha kipaza sauti wakati mgeni rasmi akizungumza wakati wa
maashimisho hayo.
Wageni waalikwa wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi (hayupo pichani)
wakati wa kumbukumbu ya maashimisho ya miaka 19 ya mauaji ya Kimbari
Rwanda.
Kaimu Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Bw. Jama Gulaid ambaye
pia ni Mkurugenzi Mkazi wa UNICEF akizungumza wakati maadhimisho ya
miaka 19 ya mauaji ya Kimbari nchini Rwanda yaliyofanyika jijini Dar es
Salaam leo katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City ambapo amesema
dunia nzima itakuwa na siku maalum ya kukumbuka wahanga wa mauaji ya
Kimbari ya Rwanda kwa heshima ambayo ni alama ya kukumbuka athari za
mauaji hayo na kuwa pamoja na walionusurika na kwa namna nyingine ni
alama msingi ya kupongeza hatua zilizochukuliwa na jamii ya Wanarwanda
kuungana pamoja.
Katika mazungumzo yake alinukuu maneno yaliyozungumzwa na Katibu Mkuu
wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon " Katika maasdhimisho ya 19 ya mauaji ya
Rwanda tunawakumbuka watu zaidi ya 800,000 wasio na hatia ambao
walipoteza maisha yao na tutanendelea kuwaheshimu walionusurika na
tutaendelea kuwa nao pamoja na kukemea wale wote waliohusika na tukio
hilo, na kuwapongeza waliojitokeza kuzuia mauaji hayo yasiendelee".
Balozi wa Rwanda nchini Tanzania Mh. Benjamin Ruganganzi akitoa salamu
zake kwa wageni waalikwa pamoja na watu waliohudhuria maadhimisho ya 19
ya mauaji ya Kimbari ya Rwanda na kuhakikisha kuwa wananchi wa Rwanda
wataendelea kudumisha uhusiano na ushirikiano pamoja na nchini zingine
za Afrika Mashariki ili kuhakikisha tukio kama hilo halitajirudia tena.
Sehemu ya wageni waalikwa wakiwemo mabalozi mbalimbali wakimsikiliza Balozi wa Rwanda nchini (hayupo pichani).
Msemaji wa Mahakama ya Umoja wa Mataifa ya Mauaji ya Rwanda (ICTR) Bw.
Roland Ammousouga akitoa kauli yake wakati wa maadhimisho ya 19 ya
mauaji ya Kimbari ya Rwanda ambapo amesema kwa miaka 19 iliyopita watu
wanaweza wakajisifu kazi iliyofanywa na mahakama ya ICTR kwamba
imetimiza kilio cha maelefu ya waathirika na kuwa imesaidia katika
kuleta upatanishi na kuijenga upya Rwanda sambamba na kuhamasisha amani
na ulinzi katika ukanda wa Afrika wa maziwa makuu, wakati haikufanikiwa
kuwakamata wale wote waliohusisha na mauaji hayo kwa kutoa itumia Rwanda
kuwatafuta wahusika 6 waiojulikana walipo ili waweze kukabiliana na
kesi zinazowakabili kinachojionyesha hapa ni kwamba ICTR inaashiria
kwamba mapambano dhidi ya mazingira ya wahusika wengine 3 hawawezi
kukamatwa.
Umati wa watu waliofurika (chini) katika maadhimisho hayo wakiwemo wanafunzi wa shule ya sekondari Jitegemee (juu).
Mmoja wa viongozi wa Dini akiomba dua ya kuwarehemu walipoteza maisha katika mauaji ya Kimbari yaliyotokea nchini Rwanda.
Meza kuu ikiongozwa na mgeni rasmi Dr. Salim Ahmed Salim kuwasha
mishumaa ikiwa ni ishara ya kuwakumbuka watu waliopoteza maisha wakati
wa mauji ya Kimbari nchini Rwanda.
No comments:
Post a Comment