Saturday, March 23, 2013

MBATIA ATAKA ANALOGIA IRUDI,,, ASEMA DIGITALI IMEATHIRI MCHAKATO WA KATIBA MPYA


Mwenyekiti wa NCCR -MAGEUZI Mh James Mbatia akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) jana katika Ofisi Ndogo ya Bunge jijini Dar es Salaam.


Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi Mh, James Mbatia ameitaka serikali ya jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Kuacha Ubabe kwakusema kuwa hakuna uwezekano wa kuwasha tena Mitambo ya Analogia kwani kitendo cha kuhama kutoka Analogia kwenda Digitali kumeathiri kwa kiwango kikubwa Mchakato wa Kutafuta Maoni ya KatibaMpya.

Ameyasema hayo jana wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katikaOfisi ndogo za Bunge zilizopo jijini Dar es Salaam.

Mbatia amesema kuwa Kabla ya kuhama kutoka Analogia Watanzania wengi walikuwa wanapata elimu juu ya mchakato wa katiba mpya tofauti na sasa ambapo wanaofaidi ni wale wachache tu wenye uwezo wa kununua Vin’gamuzi.

Kutokana na hayo, ameishauriSerikali, kusitisha kuzima Mitambo ya analojia katika mikoa ambayo bado Mitambo hiyo haijazimwa ili wawape muda wananchi wa kuweza kujiandaa kumudu kununua Vin'gamuzi hivyo.

Aidha ameitaka Serikali kuangalia mara mbili swala la kuwasha tena mitambo ya Analogia katika jiji la Dar es Salaam kwani kitendo cha kuzima Mitambo hiyo kimewanyima Watanzania wengi haki ya kupata habari.
Waandishi wa habari wakiwa makini kabisa na kazi yao wakati Mh Mbatia anazungumza

No comments:

Post a Comment