Saturday, March 23, 2013

KIATU AINA YA 'KAMONGO' KILIVYOMPONZA DAVID BECKHAM CHINA

BEIJING, China

PICHA mbalimbali zikimuonesha nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya England, David Beckham, akijaribu kuwaonesha watoto wa Kichina na Wakufunzi wa timu yao, ufundi wake wa kupiga mipira iliyokufa ‘free-kick,’ wakati akiwa ziarani hapa. 

Ufundi wa Becks haukuonekana ndani ya kiatu cheusi cha kutokea 'Kamongo' alichovalia na suti yake ya kijivu, kwani aliteleza wakati akipiga na kuanguka kama anavyoonekana. 

Ingawa alipigwa mweleka huo ambao ungevuta hisia za wengi wakati wa tukio, Wachina hawakumwangalia, badala yake waliangalia mwelekeo wa mpira huo kuona kama amefanikisha kutikisa nyavu kama kawaida yake?

No comments:

Post a Comment