Mwenyekiti wa klabu ya soka ya
Simba ya jijini Dar es salaam Ismail Aden Rage amewaomba radhi wanachama
wa klabu hiyo kwa kuwaambia kuwa kikao walichokaa Jumapili katika
katika ukumbi wa statlight ni cha harusi .
Akiongea kwa njia ya simu
katika kituo kimoja cha radio Rage amesema kuwa anaomba Radhi kama kuna
alimuudhi kwa kutumia lugha ambayo imeoneka sio nzuri Aden alikiita
kikao hicho cha wanachama hao kuwa kikao cha harusi jambo lililo zua
mijadara na kutokuelewana na baadhi ya wanachama na wengi wao kuudhiwa
na kauli kiasi kufikia kumjibu kuwa yeye atakaa cha kitchen Party .
Mwenyekiti huyo ambaye anarejea
kesho kutoka Nchini India alipokwenda kufanyiwa matibabu ya uti wa
mgongo amesema pindi atakapofika atazungumza na waandishi wa habari
kuhusu mustakbari wa klabu hiyo yenye makao yake makuu msimbazi jijini
Dar es salaam.
Kwa upande mwingine Aden
ameipongeza klabu ya Azam kwa kufanya ufunguzi wa kujenga kiwanja kipya
cha kisasa cha mpira wa miguu kilicho funguliwa leo na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete.
Ameongeza kuwa litakuwa somo
kwa klabu ya Simba na Yanga kwani japokuwa na ukongwe wa vilabu hivyo
hata majengo yao yapo katika hali mbaya .
No comments:
Post a Comment