Rais wa Shirikisho la Wahandisi la Kimataifa Ulimwenguni (FIDIC), Geoff French (kushoto), akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Ofisi ya Wahandisi Washauri Kanda ya Afrika Tanzania katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam leo. Kulia ni Rais wa Taasisi ya Wahandisi Washauri Tanzania (ASET), ambayo ipo chini ya FIDIC. Mhandisi Menye Manga. (Picha habari na www.mwaibale.blogspot.com) |
Na Dotto Mwaibale
TAASISI ya Wahandisi Tanzania (ASET),
imezindua ofisi za Kanda kwa Bara la Afrika ambayo makao yake makuu ni
Dar es Salaam chini ya uongozi wa Watanzania.
Akizindua ofisi hizo Rais wa Kanda ya
utendaji ya shirikisho la kimataifa la wahandisi washauri (FIDIC),
Geoff French, alisema lengo ni kutaka wahandisi wa Tanzania watambulike
ndani na nje ya nchi katika shughuli zake.
“Hii ni ofisi yetu ya kwanza
kufunguliwa katia mikoa mitano Tanzania ambayo itakuwa inaendeshwa na
Mtanzania katika shughuli zake zote pia atashirikiana na viongozi
wengine kutoka katika mikoa mingine,”alisema French.
Alisema wamepanga mikakati mbalimbali
katika taasisi hiyo, ikiwemo kutoa mafunzo kwa wahandisi wazawa kutokana
na changamoto za teknolojia ambazo zinazoikabili ulimwengu kutokana na
idadi ndogo ya wahandisi ambao hawatoshelezi kukidhi mahitaji ya nchi
katika kipindi hiki cha sayansi na teknolojia.
Alisema kamati ya utendaji ya Shirikisho la kimataifa la wahandisi washauri
( FIDIC), wameona kuwa ni vyema kuwa na ofisi zake hapa nchini kwani itakuwa ni heshima kubwa kwa Tanzania kutokana na amani iliyopo.
( FIDIC), wameona kuwa ni vyema kuwa na ofisi zake hapa nchini kwani itakuwa ni heshima kubwa kwa Tanzania kutokana na amani iliyopo.
Naye Rais wa Wahandisi Washauri Tanzania (ACET), Menye Manga, alisema zipo changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili katika taasisi hiyo ikiwemo kutojijengea uwezo wa kufanya kazi vizuri pamoja na kutokuwa na wahandisi wa kutosha nchini.
Tumepanga mikakati mbalimbali katika taasisi hii kwa ajili ya kuwaendeleza wahandisi wazawa ikiwemo kuwapa mafunzo pamoja na kutoa fursa ya wahandisi wengi katika suala la ujuzi wa kazi hii.
“Mafunzo hayo yatatolewa kwa mhandisi yeyote atakayependa kujiandikisha kwa ajili ya kupata ujuzi zaidi katika kazi yake ambapo mafunzo hayo yatatolewa kwa muda wa siku mbili.
“Taasisi yeyote itakayopenda kupata mafunzo hayo wanauwezo wa kuwachukua walimu hao na kuwapa mafunzo hayo kwa muda wa siku tatu au zaidi.
“Ni bora tutoe mafunzo kwa wahandisi kwani kadri siku zinavyoenda wasomi wengi wanapungua kusoma masomo ya sayansi na hisabati,” alisema Manga.
Alisema gharama za mafunzo hayo zitapungua au kuongezeka kulingana na wakufunzi watakaotoa mafunzo hayo kutoka sehemu mbalimbali duniani kama vile Dubai.
Alisema wakufunzi kutoka nje ya nchi watatoa mafunzo hayo kwa gharama ya dola za Marekani 2,000 na wale watakaotoka Tanzania watatoa kwa gharama ya dola za Marekani 850.
Aidha Manga aliwataka wahandisi waliopo Serikali za Mitaa, Jiji na Wilaya kujiandikisha katika mafunzo hayo ili waweze kupata elimu ya kutosha juu ya uhandisi.
No comments:
Post a Comment