Mkuu wa Wilaya ya Ilala |
Manispaa ya Ilala imefanikiwa kuzoa 50% kati ya takataka zote zilizopo katika Manispaa ya Ilala kwa Kipindi
cha Mwaka 2005-2012
Hayo yamesemwa Leo na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw, Raymond
Mushi, wakati alipokuwa akielezea
mafanikio ya Serikali ya awamu ya nne
kwa kipindi hicho katika wilaya hiyo.
Mushi amesema kuwa, Kiwango cha uzoaji taka ngumu kimefikia
tani 550 kwa siku sawa na tani 198,000 kwa Mwaka ambapo amesema kiwango hicho
ni asilimia 50% ya tani 1100 za taka zianazo zalishwa kwa siku.
“Kwa sasa kiwango cha
Uzoaji taka ngumu kinaridhisha kutokana na wilaya kupata vitendea kazi
vyenye uwezo Mzuri”, amesema Mkuu wa Wilaya.
Amesema kuwa
Mafanikio hayo, ni Miongoni mwa Mafanikio Mengi ambayo Serikali hiyo
imeyafikia kwa kipindi chake tangu imeingia Madarakani na kusema kuwa wana matumaini kuwa mpaka kufikia mwaka 2015,
Manispaa hiyo itakuwa imefanikisha Mengi.
Ameendelea kusema kuwa,
kufanikiwa kwa asilimia hizo kunachangiwa na kununuliwa kwa Magari sita ya kukandamiza
taka yenye Uwezo Mkubwa wa kubeba kati ya tani kumi hadi 24 kwa Safari moja
ikiwa ni pamoja na Kununuliwa kwa makasha ya taka 30 na kuwekwa kwenye maeneo
yenye uzalishaji Mkubwa wa taka.
Ameendelea kuyataja Mafanikio mengine yaliyopo katika
Manispaa hiyo kwa kipindi cha mwaka 2005-2012 kuwa ni, Usambazaji maji ambapo
amesema katika Mamlaka ya maji DAWASA imeongeza visima virefu vya Maji kutoka
visima 110 mwaka 2005 kufikia 195 na visima vifupi 60 kwa mwaka 2012.
Amesema kuwa, mafanikio hayo yameambatana na Uboreshwaji wa Huduma za Afya, Ardhi, Kilimo Ujenzi pamoja
na Elimu, ambapo Katika Afya Manispaa imefanikiwa kuongeza idadi ya Vituo vya
kutolea huduma kutoka 15 hadi 22 pamoja
na Zahanati 20 kutoka 13 zilizokuwepo kwa mwaka 2005-2012.
Waandishi wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya na kuandika mambo muhimu |
“Katika Elimu
zimeongezwa shule za Awali kufikia shule 128 tofauti na ilivyokuwa 2005
ambapo kulikuwa na shule 75 tu, pia Manispaa
imeongeza madarasa katika shule
za msingi pamoja na kuongeza shule za Sekondari ambapo kwa sasa zipo shule 49 zinazomilikiwa na Serikali na shule 42
zisizo za Serikali” amesema.
Hata hivyo katika Sekta ya Ardhi, amesema kuwa jumla ya
Viwanja 5,986 vimepimwa kwa matumizi mbalimbali ya Ardhi pamoja na Leseni
28,763 kurasimisha makazi katika maeneo mbalimbali yasiyopimwa, na amezungumzia pia swala la ujenzi an kusema
kuwa kipindi cha 2005-2012 Manispaa imeshuhudia kuwepo kwa Ujenzi mkubwa wa
Miundombinu wa Barabara Makaravati, Mifereji ya maji ya Mvua na njia za
Watembea kwa Miguu.
Aidha Bw, Mushi amesema kuwa, Mafanikio Mengine yameonekana katika sekta ya
Ajira kwa Vijana, Kilimo, vyama vya
Ushirika, Ajira za Vijana,Shughuli za Kiuchumi na Ujasiria Mali pamoja na
Utawala Bora.
No comments:
Post a Comment