Wednesday, January 30, 2013

TCRA YATANGAZA NEEMA KWA WATUMIAJI WA SIMU ZA MKONONI,,, KUANZIA MACHI MWAKA HUU GHARAMA ZA KUPIGA SIMU ZITASHUKA

Mkurugenzi wa TCRA Prof John Nkoma akifafanau jambo kwa waandishi wa habari leo katika makao makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA
 
Mkurugenzi wa mamlaka ya mawasiliano nchini (TCRA) Profesa  JONH NKOMA amesema bei za mwingiliano wa simu nchini zimeshuka kutokana na mawasiliano kuwa juu na kusababisha watu wengi kushindwa kumudu gharama hizo.

 Profesa  NKOMA ameyasema hayo jijini dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu bei za mwingiliano wa simu ambapo amewataka wamiliki wa makamupuni ya simu kuwa na viwango sawa ili  kila mtu aweze kumudu gharama za matumizi ya simu.

 Amesema Bei za kupiga simu kutoka mtandao mmoja wa simu  kwenda mwingine nchini Tanzania imeshuka kwa asilimia 66%  kutoka shilingi 113 kwa mwaka wa 2004 hadi kufikia shilingi 34.92 kwa mwaka  wa 2012.
  
        Profesa  NKOMA amesema bei za mwingiliano wa simu hazipangwi na mamlaka ya mawasiliano Tanzania bali ushindani katika mitandao ya simu ndio  huamua bei na  mamlaka  ina kazi ya kudhibiti bei hizo ili zisiwe kero kwa watumiaji ambao ni watanzania kwa ujumla.

 Profesa  NKOMA ametoa onyo kwa mitandao yote ya simu ambayo itayokiuka agizo hilo la mamlaka hiyo la kupunguza viwango hivyo vya simu kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine kwamba watahakikisha sheria inafwatwa na hatua zitachukuliwa kwa watakaokiuka tamko hilo.

 Hata hivyo ameongeza kuwa bei hizo zitazidi kupungua hadi kufikia hadi shilingi 26.96 kwa mwaka wa 2017.


No comments:

Post a Comment