WAZIRI wa Chakula na
Ushirika, Christopher Chiza amewagiza wakuu wa mikoa kutumia madaraka
waliyonayo kwa kuwachukulia hatua za kisheria mawakala watakaouza unga
kinyume na bei elekezi ya sh 750 hadi 900 kwa kila kilo.
Chiza alisema hao wakati
alipokuwa akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu
hali ya upatikanaji wa chakula nchini.
Alisema serikali imeidhinisha
kuuzwa tani 40,000 za mahindi kwa mawakala, kutoka katika ghara la
chakula la taifa kwa ajili ya maeneo yenye upungufu wa chakula, kwa bei
ya sh 450 kwa kila kilo ambapo zoezi hilo limekwisha anza Januari na
litaendelea hadi Machi mwaka huu.
“Lazima wakuu wa mikoa, wa
wilaya, wenyeviti wa mitaa kwa kushirikiana na wanannchi wenyewe
mshirikiane kwa pamoja katika suala zima la kudhibiti bei ya
unga”alisema.
Chiza alisema mikoa itapaswa
kuwachukulia hatua mawakala (sagishaji), ambao watabainika kuuza unga
huo kinyume na bei elekezi ya serikali.
“Mikoa itachukuwa hatua kwa
msagishaji ambaye atabainika kutumia vibaya kibali alichopewa kama vile
kuuza kibali hicho kwa msagishaji mwingine, kusafirisha na kuuza mahindi
au unga kwenye maeneo tofauti aliyopangiwa, kutosagisha na kuuza unga
ndani ya siku saba kwa mujibu wa mkataba” alisema.
Chiza aliitaja baadhi mikoa
yenye uhaba unga wa mahindi pamoja na tani walizopatiwa kuwa ni Arusha
(tani 1100), Dodoma (400), Kilimanjaro (400), Lindi (400), Mara (900),
Manyara (800).
Mingine ni Morogoro (400),
Mwanza (2500), Shinyanga (1029), Singinda (500), Tabora (1000), Tanga
(700),Mtwara (600), Pwani (700) Simiyu (1971) na Dar es Salaam (6400).
No comments:
Post a Comment