Sunday, January 20, 2013

EDO MAKATA AHAMIA NCCR-MAGEUZI ADAI HAKUFUKUZWA CHADEMA BALI ALIJIHUZULU KUTOKANA NA MACHAFU YALIYOMO

Katibu mwenezi na Mahusiano ya Umma wa NCCR-MAGEUZI Mh, Moses Machali (kulia) akimsomea Bw, Edo Makata kadi ya NCCR kabla ya kumkabidhi ili ajiunge rasmi katika chama hicho baada ya kutoka CHADEMA.
 
Hatimaye yule kijana ambaye alidaiwa kutimuliwa Chadema pamoja na kunyan’ganywa Madaraka Bw, Edo R Makata aliyekuwa  Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Mbeya ameungana na  chama cha Nccr-MAGEUZI leo katika makao makuu ya Chama hicho yaliyopo jijini Dar es Salaam.
Katika Mazungumzo yake na waandishi wa habari Bw, Makata ameyataja machafu mengi anayodai yamemfanya akihame CHADEMA na kuhamia NCCR na kukanusha kutimuliwa kwake na  badala yake alidai amejiuzulu mwenyewe kutokana na Machafu hayo.
Makete ameyataja baadhi ya  machafu yaliyopo katika chama hicho cha CHADEMA kuwa  ni, Ufisadi, Ukabila  pamoja na Ubabe wa Mwenyekiti wa Chama hicho Mh, Freeman Mbowe na kuongeza kuwa Dk Slaa anatumia Fedha nyingi kufanya Ziara kwa gharama ya CHADEMA pasipo Baraka za vikao halali vya Chama.

MAASINDA ilimuuliza Bw, Makata, kuwa ni kwanini hakuwahi kuzungumzia Machafu hayo wakati akiwa ndani ya chama na badala yake amesubiri aondoke ndipo akaamua kuyasema?
Jibu: Siku zote hata katika mahusiano ya Mapenzi mkiwa ndani ya mapenzi mtavumiliana mabaya yote lakini Mkiachana  ndio mtaanza kuyasema yale mabaya pamoja na siri zote zilizokuwa zinafanyika ndani, hivyo basi mimi nilikuwa navumilia tu lakini sasa kwasababu nimeondoka ndio maana nimeamua kuyatapika yote.
Bw, Makate alikabidhiwa kadi ya NCCR MAGEUZI rasmi leo na katibu Mwenezi wa Chama hicho Mh, Moses Machali naye Edo akaikabidhi kadi ya CHADEMA kwa  Mh, Moses Machali .

Baada ya kukabidhiwa kadi ya NCCR Bw, Edo aliamua kuitoa ya Chadema na kumkabidhi Mh, Moses Machali

Hapa Bw, Edo akifurahia Kadi yake mpya ya NCCR

Baadhi ya waandishi wa habari waliokuwemo kwenye mkutano huo wakiwa makini kusikiliza

Hii ndiyo kadi ya NCCR

Makata mwenyewe ndani ya kadi ya NCCR

Kadi ya CHADEMA aliyoirudisha Bw, Makata

No comments:

Post a Comment