Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akimpa
pole mfiwa,Mama Khadija Kusaga wakati alipofika nyumbani kwake Keko
Maghorofani jijini Dar es salaam jana.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh.
Edward Lowassa jana Jumapili jioni alikuwa ni miongoni mwa waombolezaji
waliofika kuaga mwili wa Marehemu Sufiani Bakari Kusaga,Nyumbani kwake
Keko Maghorofani jijini Dar es salaam.
Marehemu Sufiani Bakari Kusaga alikuwa ni mume wa Mbunge
wa zamani wa Jimbo la Temeke ambaye sasa hivi ni Katibu wa CCM
Kishapu,Mh. Khadija Kusaga.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akimfariji mfiwa,Mama Khadija Kusaga.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwa
katika mazungumzo na Mbunge wa sasa wa Jimbo la Temeke,Mh. Abbas Mtemvu
wakati walipokuwa kwenye msiba huo jana jioni.
No comments:
Post a Comment