Tuesday, November 20, 2012

WANAJESHI WALIOMUUA MTOTO WA CHIFU FUNDIKIRA WAHUKUMIWA KIFO LEO

Swetu Fundikira alipokuwa hosipitalini 
Ile kesi iliyokuwa mahakama Kuu ya kanda ya Dar es Salaam iliyokuwa inashughulikia kesi ya Marehemu Swetu Fundikira Mtoto wa  aliyekuwa Chifu Abdallah Fundikira, imefikia Tamati leo hii baada ya watuhumiwa hao watatu kuhukumiwa hukumu nzito ya Kunyongwa mpaka kufa.

Watuhumiwa hao waliohukumiwa katika mauaji ya Swetu Fundikira, ni  MTM 1900 Sajenti Roda Robert (42) wa kikosi cha JKT - Mbweni na MT 75854 Koplo Ally Ngumbe (37) wa JWTZ-Kunduchi.

Wanajeshi hao walimuua Swetu Fundikira kwa kukusudia tarehe 23 Januaru 2010 saa moja usiku katika Barabara ya Mwinijuma Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Kabla ya Kuuawa Swti alikuwa kwenye kumbi za Starehe Mango Garden akiwa na Rafiki yake Beny Kinyaiya.

No comments:

Post a Comment