TAASISI za Fedha zimeshauriwa
kuhakikisha kuwa wanapeleka huduma zao hata Vijijini kwa kuwa asilimia
kubwa ya wananchi wa Vijijini hawana uelewa wa kutosha juu ya matumizi
ya Taasisi hizo za fedha hali ambayo nayo inachangia kukithiri kwa
changamoto mbalimbali zikiwemo za matumizi mabaya ya fedha na mali
Kauli hiyo imetolewa mjini hapa na wakati
alipokuwa akiongea na Walimu mbalimbali ambao ni wadau wa Benki ya NMB
katika Siku ya Mwalimu iliyoazimishwa na Benki hiyo.
Kagenzi alisema kuwa kwa sasa
Taasisi nyingi sana za fedha zimejikita zaidi kwenye maeneo ya Mijini
huku kwa upande wa Vijijini wakiwa wamesahulika ingawaje kijijini ndiko
kwenye fursa nyingi sana za Fedha ambazo zimesahulika sana hali ambayo
nayo inachangia sana Umaskini.
Aliongeza kuwa Taasisi hizo za
Fedha zinatakiwa kubadilisha na kuimarisha mifumo zaidi hasa Vijijini
ambapo kuna fursa nyingi lakini hazitambuliki kutokana na wananchi
kushindwa kujimudu kimaisha lakini kama Taasisi za Fedha zingejikita
zaidi basi hata uchumi wa vijiji pamoja na Mikoa ingeweza kuimarika sana
na kufanya hata kiwango cha uzalishaji kuwa kikubwa sana.
“Kwa sasa hasa ndani ya Mkoa wa
Arusha Mjini unakuta kila mahali ni benki lakini ukija vijijini hakuna
hata benki ya kugeresha maisha sasa hawa Wamiliki wa Mabenki na Taasisi
za Fedha wanasahau kuwa ambaye anaweza kujikwamua zaidi kiuchumi ni mtu
wa Kijijini kwa kuwa ndani ya Vijiji kuna fursa Nyingi sana hasa za
Kilimo, na Ufugaji hivyo basi napenda kuwakumbusha kuwa mnatakiwa
kuwakumbuka hata wananchi wa Vijijini hata kwa kuwapa elimu ya kumiliki
fedha”aliongeza Bw Kagenzi
Pia alisema kuwa mbali na Mabenki
hayo kuweza kuwekeza zaidi Vijijini lakini nao wafanyakazi hasa ambao
ni waajiriwa wa Serikali wanatakiwa kuijiendeleza kwa kuhakikisha kuwa
wanatumia fursa mbalimbali za Mabenki hasa NMB kwa kuhakikisha kuwa
wanakopa na kisha kufanyia Mikopo yao kazi za maendeleo kwa manufaa ya
Jamii zao.
Awali Meneja wa Benki hiyo kwa
kanda ya Kaskazini bi Vicky Bishubo alisema lengo halisi la
kuwakutanisha walimu wa shule mbalimbali ni kuweza kuwapa elimu
mbalimbali ikiwemo huduma zinazotolewa na Benki hiyo hali ambayo
itawafanya wadau hao kuweza kufikia malengo yao mbalinbali ya Kimaisha.
“Kama tunavyojua ni kuwa benki
yetu mpaka sasa imeshatoa mikopo mingi sana kwa walimu na walimu ni
wadau wetu wa muhimu sana sasa tunapowakutanisha hivi katika siku ya
Mwalimu ndani ya benki hii tunaweza kuwaongezea uwezo wa kutumia fursa
zilizopo ambazo kama nazo watazitumia vema basi wataweza kufikia malengo
yao mbalimbali’aliongeza Bi Vicky

No comments:
Post a Comment