Wanafunzi wa Chuo kikuu cha Kampala ( KIU) kilichopo jijini Dar es Salaam wameulalamikia
uongozi wa chuo hicho kutokana na unyanyasaji wanaoupata wakiwa chuoni hapo.
Wakizungumza na MAASINDA kwa Masharti ya kutotaka majina yao
yaandikwe mtandaoni wanafunzi hao wamesema kuwa moja ya unyanyasaji unao wakera
ni kulipa Ada yao kwa mfumo wa Dola jambo ni kinyume na sera za Taifa hasa upande wa
matumizi ya Sarafu katika huduma za jamii.
Walisema kuwa jambo la wao kulipa kwa mfumo wa Dolla litawezekana
pale Taifa litakapoazimia matumizi ya Dolla (U$) katika shughuli za kawaida
kama ilivyofanyika Nchini Zimbabwe.
“Taarifa za jambo hili limeshafikishwa kwenye Vyombo husika
na mamlaka husika hazina sababu ya kukwepa uwajibikaji. Mfumo huu wa kulipa kwa
kutumia Dollar haukubaliki na hauna uhalali wowote katika ardhi ya
Tanzania kwani ni Matusi na Unyonyaji wa kupe kama sio ukupe na ujuha. Jambo
hili litawezekana pale tu sera na regulation na hata sheria au Taifa na
watanzania kuamua vinginevyo.”
Aidha wanafunzi hao wamesema kuwa Ada zao pamoja na kwamba wanalipa kwa mfumo
wa Dolla bado hazina kiwango maalum ambapo wamesema kuwa kuna mfumo
ulioanzishwa wa kulipa ada ya ziada maarufu kama Other fees ambayo wanafunzi hao
wanasema kuwa wananyonywa kutokana na
pesa hizo.
“Kila mwanafunzi hutakiwa kulipa Dollar 230 kwa semister.
Hivyo mwanafunzi mmoja huwajibika kulipia Dollar 460 kwa muhula wa masomo
ambazo ni sawa na Tsh: 736,000/= hii ni kwa hesabu ya mwanafunzi mmoja tu”,
alisema mwanafunzi mmoja.
Balaa linakuja pale mwanafunzi anapolazimishwa kulipa kiasi
hiki cha pesa kila mwaka wa masomo. Hii inamaana mwanafunzi anayeingia mwaka wa
tatu atakuwa amelipa Tsh/=1,840,000/= kiasi anacholipa mwanafunzi mmoja
ukizidisha kwa idadi ya wanafunzi 2000 wa KIU watakuwa wametapeliwa Tsh
3,680,000,000/= ambazo ni mabiloni ya fedha za kitanzania
Kwa upande wa other fees, pekee wanafunzi 2000 wa KIU
watakuwa wametapeliwa zaidi Tsh billion 3 kiasi hiki na malipo haya
yanawezekana kufanywa na wanachama wenye hisa katika kampuni au matembezi ya hisani.
Walisema kuwa Mchango
huo huongeza mzigo wa Ada isiyo na
ulazima kwa asilimia 28.409 kwa kila semister ambayo ni sawa na Tsh: 368,000/=
kwa kila semister moja.
Maasinda ilijaribu kuutafuta Uongozi wa Chuo hicho lakini jitihada
zetu hazikufanikiwa baada ya namba ya Simu tuliyopewa na chanzo chetu kuita
pasipo kupokelewa ambapo MAASINDA ilipiga namba hiyo kwa muda wa siku mbili na
haikupokelewa na tuilipo jaribu tena namba hiyo ilikuwa haipatikani.
No comments:
Post a Comment