Tuesday, November 13, 2012

MKUTANO WA KUJADILI NAMNA YA KUTUMIA NAMBA MOJA KUPIGA MITANDAO YOTE KUFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM

Mkurugenzi  Mtendaji wa Mamlaka ya  Mawasiliano Tanzania Prof John Nkoma akizungumza na waandishi wa habari leo katika  Makao makuu ya ofisi hizo ambapo alizungumzia juu ya kuwepo kwa Mkutano wa siku mbili wa kujadili juu  ya namna ya  kutumia namba moja ya simu kwenda namba nyingine.
 
Prof Nkoma amesema kuwa  zoezi hilo likifanikiwa itamwezesha mteja  kutumia namba moja tu na kuweza kuwasiliana na mitandao mingine.

Amesema kuwa mkutano huo utafanyika Tarehe 15 na 16 mwezi huu katika ukumbi wa Mikutano Mlimani City jijini Dar es Salaam ambapo mkutano huo utahudhuriwa na Makampuni Mbalimbali yakiwemo ya simu  na nchi nyingine za Jirani
Prof Nkoma akiongea na waandishi wa Habari leo katika makao makuu ya Ofisi hizo jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment