Monday, November 12, 2012

TUNATAKA KUWA NA MAAMBUKIZI YA UKIMWI SIFURI: BI JOAN CHAMMUNGU


Mwenyekiti wa Tanzania AIDS Forum Bi, Joan Chammungu, akizungumza na waandishi wa Habari jana ambapo alikuwa anazungumzia malengo mbalimbali ya Taasisi yao ambapo alisema kuwa lengo lao kubwa ni kuhakikisha kuwa Gonjwa la Ukimwi linakwisha kabisa nchini Tanzania.Bi, Chamungu alisema kuwa wamefanikiwa kuhakikisha kuwa  Maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa Mtoto yamepungua na sasa wanataka kuhakikisha kwamba Mama anaishi ili aweze kumlea yule mtoto kwa lengo la kujenga Taifa Imara.

 Aidha alizungumzia pia swala la Unyanyapaa kwa waathirika jambo ambalo linawakatisha waathirika wa Ukimwi Tamaa na kusema kuwa anawaomba waathirika kuhakikisha kuwa wanaishi na waathirika wa UKIMWI pasipo kuwanyanyapaa bali waishi nao kwa kuwatia moyo.

Alisema moja changamoto iliyopo ni kuwa Wazazi hawatoi Elimu ya kujamiiana kwa watoto jambo linalowasababisha watoto kupata Elimu hiyo kwa watu wa nje wanaosababisha watoto hao kuharibika zaidi na hatimaye kujiingiza katika maswala ya Ngono Mapema pasipo kujua hivyo amewataka wazazi watoe Elimu hiyo kwa Watoto wao.


Bi, Joan Chamungu akiwa katika mkutano wa wadau wa Ukimwi jana  katika Hoteli ya Blue Pearl jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment